Habari za Punde

Viongozi wa ADC Wazungumza na Waandishi wa Habari Wa Vyombo Mbalimbali Zanzibar.

Naibu Katibu Mkuu ADC Queen Alithbet Sendiga akizungumza katika Mkutano na Waandishi wa Habari kuhusiana na Chama hicho kuwapa kipaumbele wanawake mkutano uliofanyika ukumbi wa Sanaa Rahaleo Zanzibar.
Katibu Mkuu Taifa Chama cha ADC Doyo Hassan Doyo akizungumza na Waandishi wa Habari kuhusiana na Mkutano Mkuu wa Chama hicho Utakaofanyika Tarehe 14/04/2019 katika Hoteli ya Madinatul Bahar Chukwani  Wilaya ya magharibi B Unguja ,hafla iliofanyika katika ukumbi wa Sanaa Rahaleo Zanzibar
Katibu Mkuu Taifa Chama cha ADC Doyo Hassan Doyo akisisitiza jambo wakati akizungumza katika Mkutano na Waandishi wa Habari kuhusiana na Mkutano Mkuu wa Chama hicho utakaofanyika 14/04/2019 katika Hoteli ya Madinatul Bahr Chukwani Wilaya ya Magharibi B Unguja. mkutano uliofanyika ukumbi wa Sanaa Rahaleo Zanzibar.
Baadhi ya Waandishi wa Habari waliohudhuria katika Mkutano wa Chama cha ADC kuelezea juu ya Mkutano Mkuu wa Chama hicho14/04/2019.hafla iliofanyika ukumbi wa Sanaa Rahaleo Zanzibar.
Picha na Yussuf Simai - Maelezo Zanzibar.

Na Rahma Khanis       Maelezo Zanzibar    10/4/2019
Katibu Mkuu wa Chama Taifa  (ADC) Doyo Hassan Doyo  amemuomba Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kuwadhibiti wanasiasa wasiofuta sheria na maadili ya vyama hivyo ili kuepukana na Migogoro inayoweza kujitokeza.
Ameyasema hayo wakati akizungumza na Waandishi wa Habari katika  Ukumbi wa Sanaa Rahaleo Mjini Zanzibar.
Amesema wanasiasa ni vyema kufuata Sheria  na Kanuni zilizowekwa ili kufikia malengo na kujiepusha na migogoro isiyokuwa yalazima kwani kufanya hivyo kutapelekea kuimarisha Chama na kufikia malengo.
Lengo la Mkutano huo ni kuwapa taarifa wananchi na Wazanzibar  kuhusiana na  maandalizi ya Mkutano Mkuu wa Chama unaotarajiwa kufanyika  tarehe 14 mwenzi huu katika Ukumbi wa Madinatul Bahari Uliyopo Chukwani  Nje kidogo ya Mji wa Zanzibar.
Aidha amesema katika Mkutano huo Mkuu wa Chama Taifa watazungumzia mikakati mblimbali ikiwemo Uchaguwa Mkuu na kuchagu Viongozi wa chama hicho ili kuimarisha chama na kutia hamasa kwa Wazanzibar.
Akiongezea kutaja mikakati hiyo kuzinduwa mpango mkakati wa chama ambao unajulikana kama  ADC Kaya na ADC Shehiya  kwa Zanzibar  utakao saidia kupata mafanikio na kukiendeleza chama hicho.
Nae Naibu Katibu Mkuu Taifa wa Chama hicho Queen Althbert  Sendiga amewataka akina mama kujitokeza kwa wingi na kugombea nafasi za uongozi kwani  chama chao kinatoa fursa  kwa kila mwenyeuwezo wa  kugombea nafasi hizo.
Aidha amesema ADC inaendelea kutenda fursa na  haki kwa akina mama  kutokana na kutojitokeza kwa wingi akina mama hao kipindi kilichopita.

No comments:

Post a Comment

ZanziNews Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.