Habari za Punde

MAADHIMISHO YA SIKU YA UHURU WA VYOMBO VYA HABARI DUNIANI Mei 3, 2019

Kesho ni mei 3, ambapo ni siku ya maadhimisho ya siku ya uhuru wa vyombo vya habari duniani ambapo kila mwaka maadhimisho hayo hufanyika katika sehemu mbali mbali duniani.
Maadhimisho hayo yanafanyika kutokana na umuhimu wa vyombo vya habari katika suala zima la maendeleo ya nchi lakini katika kuimarisha demokrasia Kauli mbiu ya mwaka huu ni Wajibu wa vyombo vya habari katika uchaguzi na demokrasia. Kwa upande wa Zanzibar maadhimisho hayo yanafanyika kwa kuandaliwa kwa pamoja baina ya taasisi mbali mbali za kihabari.
Maadhimisho hayo yatafanyika katika ukumbi wa baraza la sanaa uliopo rahaleo na mgeni rasmi atakuwa ni waziri wa chi ofisi ya makamu wa pili wa rais mheshimiwa Mihayo Juma Nhunga.
Maadhimisho hayo yanakwenda sambamba na juhudi za serikali za kukuza kada ya habari na kuimarisha dhana zima ya utawala bora na weledi na ufanisi katika tasnia ya habari.
Maadhimisho hayo yameratibiwa kwa pamoja na baraza la habari Tanzania, klabu ya waandishi wa habari Zanzibar, chama cha waandishi wa habari wanawake Tanzania , chama cha waandishi wa habari za maendeleo na idara ya habari maelezo.
Majadiliano ya maadhimisho hayo yatalenga katika kukuza kada ya habari pamoja na kuimarisha sekta ya habari hapa nchini Maadhimisho yataanza rasmi saa mbili kamili asubuhi.
Imetolewa na mwenyekiti kamati ya maandalizi Maadhimisho ya siku ya uhuru wa vyombo vya habari duniani
Dkt. Juma Mohammed Salum.

No comments:

Post a Comment

ZanziNews Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.