Habari za Punde

Mwenyekiti wa UVCCM Mkoa wa Tanga Awaongoza Waombolezaji Katika Mazishi ya Katibu Hamasa Kata Yaliofanyika Chumbageni Jijini Tanga.

MWENYEKITI wa Jumuiya ya Umoja wa Vijana ya Chama cha Mapinduzi (UVCCM) Mkoani Tanga Omari Mwanga kulia akiwa kwenye msiba huo katikati ni Katibu wa Jumuiya hiyo Mkoa wa Tanga Zawadi Nyambo kushoto ni Katibu wa Hamasa na Chipukizi wa (UVCCM) Mkoa wa Tanga Waziri Mohamed
MWENYEKITI wa Jumuiya ya Umoja wa Vijana ya Chama cha Mapinduzi (UVCCM) Mkoani Tanga Omari Mwanga kulia akiwa kwenye msiba huo katikati ni Katibu wa Jumuiya hiyo Mkoa wa Tanga Zawadi Nyambo kushoto ni Katibu wa Hamasa na Chipukizi wa (UVCCM) Mkoa wa Tanga Waziri Mohamed
Sehemu ya Viongozi wa Jumuiya ya Umoja wa Vijana ya Chama cha Mapinduzi (UVCCM) Mkoa wa Tanga wakiwa msibani leo
Katibu wa Hamasa na Chipukizi wa (UVCCM) Mkoa wa Tanga Waziri Mohamed akifuatilia matukio mbalimbali kwenye msiba ambapo aliyefariki alikuwa akifanya naye kazi.

MWENYEKITI wa Jumuiya ya Umoja wa Vijana ya Chama cha Mapinduzi (UVCCM) Mkoani Tanga Omari Mwanga leo amewaongoza viongozi mbalimbali wa jumuiya kwenye mazishi ya aliyekuwa Katibu wa Hamasa na Chipukizi (UVCCM) Kata ya Chumbageni Jijini Tanga Marry Dominic Dawa yaliyofanyika Bombani Muheza.

Kabla ya mwili huo kusafirishwa kuelekea wilayani Muheza aliagwa eneo la Kange Kasera Jijini Tanga ambapo Jumuiya ya Umoja wa Vijana mkoa wa Tanga walitoa salamu zao wakati wa halfa hiyo

Akizungumza wakati kuagwa mwili huo Mwenyekiti wa UVCCM Mkoa wa Tanga Mwanga aliwapa pole wafiwa na kuwataka kuwa wavumilivu kwenye kipindi hicho kigumu cha kuondokewa na mpendwa wao.

Alisema wao kama Jumuiya wapo pamoja na familia kwenye kipindi hicho kigumu huku wakimuelezea namna katibu huyo alivyokuwa mchapakazi na hodari katika utendaji wake.

Kwa kweli hapa tumepata pigo kubwa hasa ukizungatia Marry alikuwa kiongozi hodari na shupavu kwenye kuwajibika kwenye nafasi aliyokuwepo huku wakieleza mchango wake utaendelea kukumbukwa.

Hata hivyo aliwataka viongozi waliobakia kuiga mazuri yaliyofanywa na kiongozi huyo katika kuhakikisha Jumuiya hiyo inapata mafanikio makubwa .

Msiba huo ulihudhuriwa na viongozi mbalimbali akiwemo Katibu wa UVCCM Mkoa wa Tanga Zawadi Nyambo,Katibu wa (UVCCM) wilaya ya Tanga Fahad Siraji,Katibu Hamasa wilaya ya Tanga (UVCCM) Kipanga Juma,Mjumbe wa Baraza Taifa (UVCCM) Mbaruku Asilia.

Imetolewa na Jumuiya ya Umoja wa Vijana UVCCM Mkoa wa Tanga Katibu wa Hamasa na Chipukizi (UVCCM) Mkoa wa Tanga 

No comments:

Post a Comment

ZanziNews Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.