Habari za Punde

Wananchi wa Jimbo la Mahonda Wajumuika Katika Futari Ilioandaliwa na Mwakilishi Wao.

Baadhi ya Wananchi wa Jimbo la Mahonda wakijumuika pamoja katika Futari ndani ya mfungo wa Mwezi Mtukufu wa Ramadhan ambayo imeandaliwa na Mwakilishi wa Jimbo hilo Balozi Seif Ali Iddi.
Mke wa Mwakilishi wa Jibo la Mahonda Mama Asha Suleiman Iddi akijumika na Wanachi mbali mbali wa Jimbo hilo katika Futari ya pamoja iliyofanyika kwenye Ukumbi wa CCM Mkoa wa Kasazini Unaguja uliopo Mahonda.
Mwakilishi wa Jimbo la Mahonda Balazi Seif Ali Iddi akijumika na Wanachi mbali mbali wa Jimbo hilo katika Futari ya pamoja iliyofanyika kwenye Ukumbi wa CCM Mkoa.
Baadhi ya Viongozi na Wananchi wa Jimbo la Mahonda wakijumuika pamoja katika Futari ndani ya mfungo wa Mwezi Mtukufu wa Ramadhan ambayo imeandaliwa na Mwakilishi wa Jimbo hilo Balozi Seif Ali Iddi.
Baadhi ya Wananchi na Viongozi wa Jimbo la Mahonda wakifutilia nafasa zilizokuwa zikitolewa mara baada ya Futari ya pamoja kwenye Ukumbi wa CCM Mkoa wa Kasazini Unaguja uliopo Mahonda.
Naibu Waziri wa Nchi Ofisi ya Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Mh. Mihayo Juma N’hunga akitoa shukrani kwa Wamnanchi na Viongozi walioshiriki Futari ya Pamoja kwa niaba ya Balozi Seif.
Picha na – OMPR – ZNZ.
Na.Othman.Khamis OMPR.
Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Balozi Seif Ali Iddi alisema kwamba kitendo cha Waumini wa Dini ya Kiislamu kukubali kuitikia mualiko wa kufutari pamoja  unaotolewa na mmoja kati yao ni jambo la faraja linaloleta mapenzi  katika Ibada ya Funga ya Mwezi Mtukufu wa Ramadhan.
Balozi Seif Ali Iddi alitoa nasafa hizo katika Shukrani zilizotolewa kwa niaba yake na Naibu Waziri wa Nchi Ofisi ya Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Mh. Mihayo Juma N’hunga mara baara ya Futari ya pamoja iliyowakutanisha Viongozi, Wakaazi na Wananchi wa Jimbo la Mahonda hapo Ukumbi wa CCM Mkoa Mahonda Mkoa Kaskazini Unguja.
Futari hiyo ambayo ni utaratibu aliyojiwekea Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar kuufanya katika maeneo mbali mbali Nchini imefanyika mwanzo mwa Kumi la Pili la Maghfira ndani ya Mfungo wa Mwezi Mtukufu wa Ramadhan.
Mh. Mihayo Juma N’hunga kwa Niaba ya Balozi Seif ambae pia ni Mwakilishi wa Jimbo la Mahonda alisema mfumo wa kukirimu Mja mwenye maisha magumu ambao umo ndani ya miongozo wa Dini husaidia kushusha baraka kwa pande zote mbili kati ya yule alicho nacho na mwenye mazingira Duni.
Akitoa shukrani kwa niaba ya Viongozi, Wakaazi na Wananchi wa Jimbo la Mahonda pamoja na wale wa Mkoa Kaskazini Unguja, Mkuu wa Mkoa huo Mh. Vuai Mwinyi alimpongeza Balozi Seif  kwa utaratibu huo aliojipangia wenye mnasaba wa kujikubalisha kuwa karibu zaidi na Wananchi wake.
Mh. Vuai alisema ukaribu wa Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Balozi Seif Ali Idi umejenga nyumba mbili bora za yakini ya moyo inayofanya kazi katika maisha ya dunia na yale maisha ya baadae yanayohitaji maandalizi mkubwa ya ucha Mungu.
Wakati waumini wa Dini ya Kiislamu wakiendelea na Ibara ya Mfungo wa Mwezi Mtukufu wa Ramdhani harakati za kujiandaa na ucha mungu ndani ya Mwezi huo kwa kusoma Qurani, Sala za Sunna, Mashindano ya kuhifadhi Quran kwa Wanafunzi wa Madrasa tofauti Nchini zimekuwa zikipamba moto.

No comments:

Post a Comment

ZanziNews Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.