Habari za Punde

Kaimu RC Tanga Akemea Vikali Baadhi ya Vyama Vya Ushirika Kufanya Ubadhilifu.

KAIMU Mkuu wa Mkoa wa Tanga Thobias Mwilapwa akizungumza wakati wa akifungua Jukwaa la tatu la Ushirika Mkoa huo 2019 lililoshirikisha wadau kutoka wilaya zote za mkoa huo lililokwenda sambamba na kauli mbiu ya Ushirika kwa kazi wenye Staha”
 Katibu Tawala Msaidizi  Uchumi na Uzalishaji Mkoa wa Tanga Benedict Njau akizungumza wakati wa akifungua Jukwaa la tatu la Ushirika Mkoa huo 2019 lililoshirikisha wadau kutoka wilaya zote za mkoa huo lililokwenda sambamba na kauli mbiu ya Ushirika kwa kazi wenye Staha”
 Mrajisi Msaidizi wa Vyama vya Ushirika Mkoa wa Tanga Jacqueline Senzighe akizungumza wakati wa Jukwaa hilo
 Mwenyekiti wa Jukwaa la Ushirika Mkoa wa Tanga Mashi Sopah akizungumza wakati wa Jukwaa hilo
 MKUU wa Idara ya Ugani na Huduma za Jamii Mhadhiri Msaidizi wa Chuo cha Ushirika (MoCU) Paulo Anania Fute akiwasilisha mada ya Elimu ya Ushirika ,Ukaguzi na Usimamizi wakati wa Jukwaa hilo
 Mhadhiri Msaidizi wa Chuo cha Ushirika Moshi ofisi ya Mkoa wa Tanga Abel Ngowi akizungumza wakati wa Jukwaa hilo
 Sehemu ya washiriki wa Jukwaa hilo
 MENEJA wa Bodi ya Korosho kulia akiwa kwenye Jukwaa hilo
 Sehemu ya wadau mbalimbali wakifuatilia hotuba ya mgeni rasmi kwenye Jukwaa hilo
KAIMU Mkuu wa Mkoa wa Tanga Thobias Mwilapwa ambaye pia ni Mkuu wa wilaya ya Tanga katikati akiwa kwenye picha ya pamoja na Katibu Tawala Msaidizi  Uchumi na Uzalishaji Mkoa wa Tanga Benedict Njau kulia na Mrajisi Msaidizi wa Vyama vya Ushirika Mkoa wa Tanga Jacqueline Senzighe mara baada ya kufungua Jukwaa hilo.


KAIMU Mkuu wa Mkoa wa Tanga Thobias Mwilapwa amekemea vikali vitendo vya baadhi ya viongozi vyama vya ushirika wanaofanya ubadhirifu huku akitaka wachukulia hatua kali ikiwemo kuwaondoa kwenye nafasi zao maana wanaweza kuwaharibia.

Mwalapwa ambaye pia ni Mkuu wa wilaya ya Tanga aliyasema hayo leo wakati akifungua Jukwaa la tatu la Ushirika Mkoa huo 2019 lililoshirikisha wadau kutoka wilaya zote za mkoa huo lililokwenda sambamba na kauli mbiu ya Ushirika kwa kazi wenye Staha”

Alisema kwamba bila kufanya hivyo viongozi wa namna hiyo wanaweza kuwa kikwazo kikubwa cha vyama hivyo kushindwa kufikia malengo yao waliojiwekea hivyo ni vema wakakaa pembeni ili kutua fursa kwa wengine ambao wanaviendeshwa kwa tija na manufaa makubwa.

“Lipo tatizo kubwa ambalo lipo kwa baadhi ya viongozi ushirika kufanya ubadhirifu kwenye vyama vya ushirika hawa tusiwafumbie macho lazima tuchukue hatua za kuwadhibiti ikiwemo kuwaondoa kwenye nafasi maana wanataka kutuharibia”Alisema Kaimu Mkuu huyo wa Mkoa.

Aidha pia aligusia tatizo sugu la ukopaji kwenye vyama hivyo huku aliwataka wanaonufaika na mikopo mbalimbali wahakikishe wanairudisha kwa wakati ili ili uweze kutumika kuwasaidia wengine

Kaimu Mkuu huyo wa Mkoa alisema wanataka ushirika uleta manufaa zaidi kwa kuwasaidia wanachama,jamii na Taifa ili yafikwe malengo makubwa ya kuweza kupata maendeleo na kuweza kujikwamua kiuchumi.

“Lakini hayo yote yaweze kufikiwa lazima mambo yaenda kwa mujibu wa sheria na taratibu ...pia nitumie jukwaa hili kukemea tabia za baadhi ya viongozi wa wabadhirufu kwenye vyama vya ushirika tuchukue hatua za kuwadhibiti ikiwemo kuwaondoa kwenye nafasi maana wanataka kutuharibia”Alisema

Alieleza pia kwamba ikiwa watu wamekopa fedha na wanashindwa kuzirudisha na kupelekea kuwa mkopaji sugu maana yake anawazuia wenzake wengi fursa ya kunufaika na mkopo huo.

Hata hivyo alitoa wito kwa vyama hivyo kuhakikisha mali za ushirika huo zinatambuliwa na zirasimishwe ili kuweza kuleta tija na kuchochea shughuli za kimaendeleo.

Awali akizungumza katika Jukwaa hilo Mrajisi Msaidizi wa Vyama vya Ushirika Mkoa wa Tanga Jacqueline Senzighe alisema vyama vya ushirika vimezidi kuongezeka na kufikia 421 na vyama vikuu vitatu huku vikiwa wanachama 61,878.

Senzighe alisema hali ya vyama ya ushirika na mikopo vinaendelea vizuri na mpaka sasa wamekwisha kutoka mikopo yenye thamani ya Bilioni 42.2 na ambayo imerejeshwa kati ya hiyo ni bilioni 31.5.

Aidha alisema changamoto kubwa wanazokabiliana nazo ni uhaba wa maafisa ushirika kutokupata mafunzo mara kwa mara kuwajengea uwezo

Hata hivyo aliongeza kwamba changamoto nyengine ni baadhi ya wenyeviti wa Serikali za Vijiji kukaataa ushirika kutokana na kujilimbikizia mali za ushirika huku wengine wakitaka mikataba ya kuuza bila utaratibu wa ushirika.

Alieleza kwamba changamoto nyengine ni uwepo wa miundombinu mibovu ambayo husababisha hasara kwa vyama vya mazao kutokana na bidhaa zao kuharibika kabla ya kufika sokoni.

No comments:

Post a Comment

ZanziNews Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.