Habari za Punde

Naibu Waziri wa Mambo ya Ndani Mhe, Hamad Masauni Atembelea Mradi wa Nyumba za Nyumba za Polisi Kunduchi,Mikocheni na Kituo Kipya cha Polisi Osterbay Jijini Dar es Salaam

Naibu Waziri wa Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi, Mhandisi Hamad Masauni (wapili kushoto), akiongozana na wataalamu kutoka Kikosi cha Uzalishaji cha Jeshi la Polisi na Wasimamizi wa Mradi kutembelea   eneo la Kunduchi ambako  Mradi wa  Nyumba Mia Tatu Thelathini za Makazi ya Polisi zinazoonekana pichani  zikiwa  zishakamilika.Ziara hiyo imefanyika  jijini Dar es Salaam
Kamanda wa Polisi Mkoa wa Kipolisi Kinondoni, ACP Mussa Taibu, akimuelekeza jambo  Naibu Waziri wa Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi, Mhandisi Hamad Masauni, wakati wa ziara ya kutembelea eneo la Mikocheni  ambako  kumejengwa  nyumba  zinazoonekana  pichani  ikiwa ni makazi kwa ajili ya  askari  polisi. Ziara  hiyo  imefanyika  jijini Dar es Salaam
Kamanda  wa Polisi Mkoa wa Kipolisi Kinondoni, ACP Mussa Taibu, akitoa taarifa  ya hali ya uhalifu katika mkoa wake kwa   Naibu Waziri wa Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi, Mhandisi Hamad Masauni, wakati naibu waziri alipofika kituo cha polisi Oysterbay. Ziara hiyo imefanyika jijini Dar es Salaam
Naibu  Waziri  wa  Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi, Mhandisi Hamad Masauni  akisalimiana  na  Kamanda  wa  Polisi  Mkoa  wa  Kipolisi Kinondoni, ACP Mussa Taibu, baada  ya  kuwasili  kwa ziara ya kikazi katika Mradi wa Ujenzi wa Kituo  Kipya  cha  Polisi  Oysterbay. Ziara hiyo imefanyika jijini Dar es Salaam.
Picha na Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi

No comments:

Post a Comment

ZanziNews Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.