Habari za Punde

Mwenyekiti wa CCM Mkoa wa Mjini Atoa Sadaka Kwa Viongozi wa Majimbo katika Mkoa huo kwa ajili ya Iddil-fitri.

Na. Takdir  Suweid -Wilaya Mjini.
Mwenyekiti wa Chama cha Mapinduzi Mkoa wa Mjini Talib Ali Talib amewaagiza Viongozi wa Majimbo wa Mkoa huo kuwashajiisha Vijana wao kuhubiri Amani na Utulivu hasa katika kipindi hiki cha Sikuu ya Idil-fitri ili kuifanya nchi ibaki kuwa salama.
Amesema kuna baadi ya Vijana wanafanya vitendo vinavyashiria uvunjifu wa Amani kama vile kufanya Fujo katika Viwanja,kuiba na kuendesha Pikipiki kwa mwendo kasi mambo ambayo yanaweza kuchafua Amani ya nchi iliopo.
Ameyasema hayo wakati alipokuwa akigawa sakaka  ya Nyama kwa Wenyeviti,Makatibu na Makatibu Hamasa wa Majimbo yaliomo ndani ya Mkoa huo,Sadaka ambayo imetolewa huko Amani Wilaya ya Mjini.
Amesema asilimia kubwa ya Vijana wanakwenda kusherehekea Sikuu katika Viwanja vya Mjini hivyo ni vyema kwa Viongozi hao kuwaeleza Vijana wao umuhimu na athari za kukosekana kwa suala la Amani na Utulivu.
Aidha amewataka kuyaendeleza mambo mema waliofanya katika kipindi cha Mwezi Mtukufu wa Ramadhani ili kunusuru kuharibu funga zao.
Nao Baadhi ya Viongozi hao wa Majimbo ya Mkoa wa Mjini wamesema Sadaka hiyo imeweza kuwasaidia katika Sikuu ya Iddil-fitri na kumuomba kutoa Sadaka hiyo kila mwaka ifikapo msimu wa Sikuu ili kuzidi kuwafariji na kuwapa moyo Viongozi hao.

No comments:

Post a Comment

ZanziNews Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.