Habari za Punde

Tanzania Yawa Mwenyeji wa Mafunzo ya Ukaguzi wa Kodi.

Mkurugenzi wa Huduma na Elimu kwa Mlipakodi wa Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA) Richard Kayombo akifungua rasmi mafunzo ya ukaguzi wa kodi ambayo yameandaliwa na TRA kwa kushirikiana na African Tax Administration Forum (ATAF). Mafunzo hayo ya wiki moja yanafanyika jijini Dar es Salaam na jumla ya wakaguzi wa kodi 50 wameshiriki mafunzo hayo kutoka Mamlaka za Mapato mbalimbali Barani Afrika.  
Meneja wa Mafunzo ya Ukaguzi wa Kodi kutoka African Tax Administration Forum (ATAF) Caroline Mutayabarwa akizungumza wakati wa hafla fupi ya ufunguzi wa mafunzo ya ukaguzi wa kodi ambayo yameandaliwa na TRA kwa kushirikiana na ATAF ambapo jumla ya wakaguzi wa kodi 50 wameshiriki mafunzo hayo kutoka Mamlaka za Mapato mbalimbali Barani Afrika.  Mafunzo hayo ya wiki moja yanafanyika jijini Dar es Salaam na yatamalizika tarehe 28 Juni, 2019.


Mkurugenzi wa Huduma na Elimu kwa Mlipakodi wa Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA) Richard Kayombo (katikati) akiwa katika picha ya pamoja na baadhi ya menejimenti ya TRA, wakufunzi na wakaguzi wa kodi mara baada ya ufunguzi rasmi wa mafunzo ya ukaguzi wa kodi ambayo yameandaliwa na TRA kwa kushirikiana na ATAF ambapo jumla ya wakaguzi wa kodi 50 wameshiriki mafunzo hayo kutoka Mamlaka za Mapato mbalimbali Barani Afrika.  Mafunzo hayo ya wiki moja yanafanyika jijini Dar es Salaam na yatamalizika tarehe 28 Juni, 2019. (PICHA ZOTE NA VERONICA KAZIMOTO)

No comments:

Post a Comment

ZanziNews Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.