Habari za Punde

Vijana Mabaraza ya Vijana Kisiwani Pemba Wapata Elimu Uongozi.

KAIMU katibu Mtendaji wa baraza la Vijana Zanzibar Khamis Faraji Abdalla, akizungumza na vijana wa kike wakati  wa mafunzo ya Uongozi kwa vijana wakike wa mabaraza ya Vijana Pemba, yaliyofanyika ukumbi wa maktaba Chake Chake.
 AFISA Mdhamini Wizara ya Vijana Utamaduni Sanaa na Michezo Fatma Hamad Rajab, akifungua mafunzo ya siku mbili juu ya Uongozi kwa vijana wa kike wa mabaraza ya Vijana Pemba, yaliyofanyika ukumbi wa maktaba Chake Chake
VIJANA kutoka bamaraza ya vijana Pemba, wakifuatilia kwa makini ufunguzi wa mafunzo ya Uongozi kwa vijana wa kike kutoka mabaraza ya vijana, yaliyotolewa na Wizara ya Vijana Utamaduni Sanaa na Michezo kwa ufadhili wa UNFPA
MRATIB wa Kituo cha Huduma za Sheria Zanzibar Tawi la Pemba Fatma Khamis Hemed, akiwasilisha mada ya ushawishi na Utetezi wakati wamafunzo ya uongozi kwa vijana wa kike wa mabaraza ya vijana Pemba, huko katika ukumbi wa Madungu Chake Chake.
(PICHA NA ABDI SULEIMAN, PEMBA)

No comments:

Post a Comment

ZanziNews Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.