Habari za Punde

Wananchi wa Manispa ya Iringa Wapongeza Utekelezaji Kazi wa Madiwani wa CCM


Naibu Meya wa Manispaa ya Iringa kupitia chama cha mapinduzi (CCM) Joseph Lyata ambae ni Diwani wa kata ya Kwakilosa akiwa pamoja na mwenyekiti wa umoja wa vijana manispaa ya Iringa Salvatory Ngerea,diwani wa kata ya Mwangata Nguvu Chengula pamoja na baadhi ya wananchi wa mtaa wa Mkimbizi A wakiwa kwenye picha ya pamoja
 Naibu Meya wa Manispaa ya Iringa kupitia chama cha mapinduzi (CCM) Joseph Lyata ambae ni Diwani wa kata ya Kwakilosa akiwa pamoja na mwenyekiti wa umoja wa vijana manispaa ya Iringa Salvatory Ngerea,diwani wa kata ya Mwangata Nguvu Chengula pamoja na baadhi ya wananchi wa mtaa wa Mkimbizi A wakiwa kwenye picha ya pamoja

Na.Fredy Mgunda - Iringa.
WANANCHI wa kata ya Mkombizi Manispaa ya Iringa wamekishukuru chama cha Mapinduzi ccm kupitia umoja wa madiwani wa chama hicho kwa kutatua kero yao ya ubovu wa miundombinu ya barabara iliyodumu kwa muda wa miaka saba.
Ni siku moja tu juni imepita   toka wananchi wa kata ya Mkimbizi Manispaa iliyopo chini ya upinzani wa chama cha demokrasia na Maendeleo chadema kutoa kero yao ya ubovu wa miundombinu ya barabara katika mkutano wa hadhara wa madiwani wa ccm wa Manispaa ya Iringa,uliofanyika juni 23 katika kata hiyo kuwaomba watengenezewe miundombinu barabara hiyo ambayo imenakwamisha shughuli za kiuchumi kutoka na ubovu wake.
Akizungumza wakati wa ukarabati wa barabara hizo Naibu Meya wa Manispaa ya Iringa kupitia chama cha mapinduzi (CCM) Joseph Lyata ambae ni Diwani wa kata ya Kwakilosa ccm alisema kuwa lengo lao ni kutaka kuhakikisha barabara zote korofi zinakarabatiwa kupitia umoja wao kwa kushirikiana na wadau wa maendeleo.
“Madiwani wa chama cha Mapinduzi ccm katika Manispaa ya Iringa tumeamua kwa umoja wetu katika kuelekea uchaguzi wa serikali za mitaa kuangalia kero zilizopo katika kata zote 18 bila kujali iko ipinzania ua chama tawala’’Alisema
Alisema kuwa  lengo  lao ni kuhakikisha kero ndogondogo za wananchi katika kata  za madiwani wa ccm ndani ya Manispaa zinatanawatumikia wananchi wananchi wanatatuliwa kero zao.
Mpaka sasa jumla ya kata  5 tumeshakarabati miundombunu ya barabara ambazo ni kata ya Mwangata,Kihesa,Mtwivila, ,Kwakilosa ,Ipogolo na leo tupo kata ya Mkimbizi,tunataka maeneo ambayo ni korofi yanafanyiwa matengenezo;
Huu mpango ni endelefu,tutaendelea katika kata zote tukiwa na lengo kubwa la kuhakikisha kata ambazo zina changamoto ya miundombinu na kero zingine zinatuliwa kwa wakati katika kelekea uchaguzi wa serikali za mitaa’’Alisema
Diwani wa kata ya Mwangata kupitia chama cha mapinduzi (CCM) Nguvu Chengula alisema kuwa  umoja wa madiwani wa ccm wameamua kupita kila kata ya diwani anaetokana na chama hicho kuangalia kero na changamoto ambazo hazijatatuliwa wanashirikiana kwa pamoja na kutatua.
Chengula alisema kuwa umoja wa madiwani wa ccm kwa  kushirikiana na wadau wa maendeleo ndani ya manispaa ya Iringa tutahakikisha tunawafikia wananchi kila kata na kusikiliza kero zao na kuzipatia ufumbuzi ili uchaguzi wa serikali za mitaa unaotarajia kufanyika nchini mwaka huu ccm iweze kushinda kwa kishindo.
‘’Mikakati tuliyojiwekea sisi kama Madiwani tunaotokana na chama cha mapinduzi ccm  ni kuhakikisha mapaka kufikia August 30 barabara zote korofi zilizopo katika kata na mitaa ya manispaa ya Iringa zinakarabatiwa ili wananchi waweze kufanya shughuli zao bila kikwazo’’Alisema
Nae mkuu wa wilaya ya Iringa Richard Kasesela aliwapongeza madiwani hao kwa kuisaidia serikali katika kutatua kero za wananchi kwa vitendo,huku akiwataka wananchi kutoa ushirikiano wa madiwani hao ili kero zinazowakabili ziweze kutatuliwa.
''Tumemuomba mh.Rais atusaidie fedha kwa ajili ya kuweka rama katika barabara za manispaa ya Iringa zenye urefu wa kilomita 21,tunaamini mh.Rais atatusaidia,hivyo ninawaomba wadau wa maendeleo kujitoa waunge mkono juhudi hizi zinazofanywa na madiwani katika kuleta maendeleo ya manispaa ya Iringa''Alisema
Kwa upande wake mwenyekiti wa mtaa wa Mkimbizi A,Agata Kasisi alisema  kuwa barabara hizo zimekuwa kikwazo kikubwa kwa wananchi hasa wafanyabiashara,bodaboda pamoja na wanafunzi ambao wamekuwa wakishindwa kwenda shule kutokana na miundombinu kutokana rafiki.
‘’Tunae diwani wa chadema aliyechaguliwa na wananchi,lakini ameshindwa kutatua changamoto mbalimbali zinazotukabili katika kata yetu ikiwemo changamoto ya miundombinu.Tunawashukuru madiwani wa ccm pamoja na chama cha mapinduzi klwa ujumla kwa kututatulia kero hii na tunahidi kosa ambalo tulilifanya katika uchaguzi mkuu 2025 hatutalirudia  katika serikali za mitaa na uchaguzi mkuu 2020’’Alisema

No comments:

Post a Comment

ZanziNews Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.