Habari za Punde

Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Mhe, Balizi Seif Ali Iddi Ajumuika na Wajumbe wa Baraza la Wawakilishi Katika Futari Maalum Iliyofanyika Katika Ukumbi wa Sheikh Idrissa Abdulwakil Kikwajuni Zanzibar. K

Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Balozi Seif Ali Iddi akijumuika na Wajumbe wa Baraza la Wawakilishi Zanzibar katika Futari ya pamoja.

Wajumbe wa Baraza la Wawakilishi wakijumuika katika Futari ya pamoja iliyoandaliwa na Mtendaji Mkuu wa Serikali Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Balozi Seif Ali Iddi hapo Ukumbiwa Sheikh Idriss Abdulwakil Kikwajuni.
Wajumbe wa Baraza la Wawakilishi wakijumuika katika Futari ya pamoja iliyoandaliwa na Mtendaji Mkuu wa Serikali Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Balozi Seif Ali Iddi hapo Ukumbiwa Sheikh Idriss Abdulwakil Kikwajuni.

Baadhi ya Mawaziri na Manaibu Mawaziri Wanawake akijumika kwenye Futari hiyo iliyowajumuisha Wajumbe wa Baraza la Wawakilishi Zanzibar.
Naibu Waziri wa Nchi Ofisi ya Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Mh. Mihayo Juma N’hunga kwa niaba ya Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar akitoa salamu kwa Wajumbe wa Baraza la Wawakilishi waliohudhuria Futaro ya pamoja.
Spika wa Baraza la Wawakilishi Zanzibar Mh. Zubeir Ali Maulid akitoa shukrani kwa niaba ya Wajumbe wa Baraza hilo baada ya Fuitari ya pamoja iliyoandaliwa na Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Balozi Seif.









Waumini wa Dini ya Kiislamu Nchini wako katika siku za mwisho za Ibada ya Funga ya Mwezi Mtukufu wa Ramadhani uliowajibishwa kwao kuutekeleza ikiwa ni nguzo ya Nne kati ya Tano za Dini hiyo.
Mwezi wa Ramadhani uliogawika Makumi Matatu huanza na lile la Rehema, likifuatiwa na Maghfira na kumalizia Kumi la Tatu la Kuachwa huru na Moto Makumi ambayo Waumini hutakiwa kujipinda katika kujikurubisha kwa Mola wao aliyeumba Dunia na vilivyomo ndani yake.
Yapo mambo yaliyosisitizwa kufanywa na Waumini hao wa Dini ya Kiislamu ndani ya Mwezi Mtukufu wa Ramadhani likiwemo lile maarufu la wachamungu hao kufutari pamoja mfumo unaowapa darasa kubwa la kuendelea kushirikiana hata katika miezi mengine ya kawadia.
Wajumbe wa Baraza la Wawakilishi, Watendaji wa chombo hicho cha kutunga Sheria pamoja na baadhi ya Wananchi na Viongozi wa Kisiasa na Serikali walipata fursa adhimu katika kufutari pamoja iliyoandaliwa na Mtendaji Mkuu wa Serikali, Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Balozi Seif Ali Iddi.
Mjumuiko huo wa Futari ya pamoja unaofanana na ile mengine katika maeneo mbali mbali Nchini umefanyika katika Ukumbi wa Sheikh Idriss Abdulwakil uliopo Mtaa wa Kikwajuni Mjini Zanzibar.
Akitoa shukrani kwa niaba ya Wajumbe wa Baraza la Wawakilishi pamoja wa Washiriki wa Futari hiyo, Spika wa Baraza hilo Mheshimiwa Zubeir Ali Maulid alimpongeza Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar kwa utaratibu wake huo wa kukusanya Makundi mbali mbali katika Futari ya pamoja.
Mh. Zubeir alisema kitendo hicho mbali ya kuleta upendo kati ya Viongozi na Makundi hayo lakini pia unasaidia kuwaunganisha pamoja Wananchi katika harakati zao za Kimaisha zinazowapa fursa ya kubadilishana uzoefu na kuzaa mbinu za kukabiliana na changamoto zinazowakabili katika katika Maisha yao ya kila siku.

No comments:

Post a Comment

ZanziNews Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.