Waziri wa Habari,Utamaduni,Sanaa na Michezo Mhe.Dkt.Harrison Mwakyembe akiangalia makombe ambayo Shule ya Sekondari ya Foutain Gate Academy wameshawahi kuyapata katika mashindano mbalimbali leo Juni 28,2019 alipofanya ziara kituoni hapo kuona namna vijana hao wanavyofundishwa Michezo mbalimbali.
Waziri wa Habari,Utamaduni,Sanaa na Michezo Mhe.Dkt.Harrison Mwakyembe (Katikati) akizungumza na wanafunzi (hawapo katika picha) ambao pia ni wanamichezo wa Shule ya Sekondari ya Foutain Gate Academy leo Juni 28,2019 alipofanya ziara kituoni hapo kuona namna vijana hao wanavyofundishwa Michezo mbalimbali.Kushoto ni Meneja wa kituo hicho Bw.Wendo Makau, na kulia ni Mkuu wa Shule ya Msingi Bw.William Tumshabe.
Mkuu wa Shule ya Sekondari ya Foutain Gate Academy Bw.Dennis Joel akizungumza leo Jijini Dodoma wakati Waziri wa Habari,Utamaduni,Sanaa na Michezo Mhe.Dkt.Harrison Mwakyembe (kulia) alipofanya ziara kituoni hapo kuona namna vijana hao wanavyofundishwa Michezo mbalimbali.
Waziri wa Habari,Utamaduni,Sanaa na Michezo Mhe.Dkt.Harrison Mwakyembe akiongozwa na uongozi wa Sekondari ya Foutain Gate Academy kukagua uwanja wa mpira wa shule hiyo leo Juni 28,2019 Jijini Dodoma alipofanya ziara shuleni hapo kuona namna vijana hao wanavyofundishwa Michezo mbalimbali.
Waziri wa Habari,Utamaduni,Sanaa na Michezo Mhe.Dkt.Harrison Mwakyembe (Katikati ) akiwa katika picha ya pamoja na Wanafunzi na Waalimu wa Shule ya Sekondari ya Foutain Gate Academy leo Juni 28,2019 Jijini Dodoma alipofanya ziara kituoni hapo kuona namna vijana hao wanavyofundishwa Michezo mbalimbali.
Na
Shamimu Nyaki -WHUSM
Waziri wa Habari, Utamaduni,Sanaa na Michezo
Mhe.Dkt.Harrison Mwakyembe amesema kuwa Serikali inatambua na kuthamini mchango
mkubwa unaofanywa na Taasisi pamoja na vituo vya kukuza vipaji katika sekta ya
michezo hapa nchini kwakua imechangia kwa kiasi kikubwa kupatikana kwa
wachezaji wengi walioliwakilisha Taifa vizuri katika mashindano mbalimbali.
Waziri Mwakyembe ameyasema hayo leo, Jijini
Dododma alipotembelea kituo cha mafunzo ya Michezo cha Foutain Gate Academy
ambapo mbali na kuupongeza uongozi wa kituo hicho na kuahidi kutafuta wafadhili
mbalimbali watakaowezesha kituo hicho kufanya vizuri zaidi.
"Mnafanya kazi kubwa sana ya kuibua na kukuza
vipaji, nawaahidi Serikali itaendelea kushirikiana nanyi pale ambapo mtakwama
ikiwemo kutuma timu ya Wataalam wa michezo kutoka Wizarani ili waje kutoa
ushauri wa kitaalam katika michezo pamoja na kupokea maoni kutoka kwenu ili kwa
pamoja tukuze sekta ya michezo"Dkt Mwakyembe.
Aidha, Dkt.Mwakyembe
ameiagiza Idara ya Maendeleo ya Michezo kufika katika kituo hicho kuona namna
mafunzo yanavyoendeshwa pamoja na kutoa elimu kuhusu taaluma za Michezo
zinazotolewa na Chuo cha Michezo cha Malya ili wakufunzi wa kituo hicho waweze
kwenda kujifunza zaidi katika chuo hicho.
Naye Mkuu wa Shule ya Sekondari hiyo Bw,Dennis Joel amesema kuwa shule hiyo
mbali na kutoa elimu,imeweka Michezo kipaumbele ili kupata vijana wengi wasomi
lakini pia wanaoweza kucheza michezo mbalimbali ambayo inaweza kuwapatia ajira.
Kwa upande wake Meneja wa Kituo hicho Bw.Wendo
Makau amesema kituo hicho kinalengo la kukuza vipaji na kuwaandaa vijana
watakaoshiriki michezo nje ya nchi kwakua vijana wengi wana ndoto ya kufikia
hatua ya kucheza nje ya nchi.
Naye Nahodha wa timu ya mpira wa miguu chini ya
umri wa miaka 20 Ramadhan Albert amesema anashukuru nafasi aliyoapata ya
kujiunga na kituo hicho kwakua ndoto zake ni kuwa mwanamichezo mkubwa ndani na
nje ya nchi.
No comments:
Post a Comment