Habari za Punde

Waziri Mkuu wa Jamuhurei ya Muungano wa Tanzania Mhe. Kassim Majaliwa Apokea Vifaa Vya Hospital na Shule Kutoka Taasisi ya Helping Hand na Benki ya NMB.

Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akipata maelezo kutoka kwa  Mkuu wa Idara ya Huduma za Serikali wa Benki ya NMB, Vicky Bishubo (wapili kulia) kuhusu kompyuta na madaftari kwa ajili ya shule wilayani Ruangwa pamoja na madirisha ya aluminium na milango kwa ajili zahanati ya Nandagala . Makabidhiano hayo yalifanyika kwenye Zahanati ya Nandagala
Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa  akizungumza baada ya kupokea vifaa mbalimbali vya hospitali kutoka Taasisisi ya Helping Hand vyenye thamani ya sh. Milioni 250 pamoja na madirisha ya aluminium, milango kwa ajili ya zahahanati ya Nandagala wilayani Ruangwa pia kompyuta na madftari kwa ajili ya shule za wilaya hiyo vyanye thamani ya sh.milioni 25 vilivyotolewa na Benki ya NMB. Makabidhiano hayo yalifanyika kwenye viwanja vya zahanati ya Nandagala
Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akiwa katika picha ya pamoja na baadhi ya wafanyakazi wa Benki ya NMB baada ya kupokea madirisha ya aluminium na milango kwa ajili ya zahahanati ya Nandagala wilayani Ruangwa pia kompyuta na  madftari kwa ajili ya shule za wilaya hiyo vyanye thamani ya sh.milioni 25 vilivyotolewa na NMB. Makabidhiano hayo yalifanyika kwenye viwanja vya zahanati ya Nandagala
Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akiwaaga wananchi baada ya kupokea vifaa mbalimbali vya hospitali kutoka Taasisisi ya Helping Hand vyenye thamani ya sh. Milioni 250. Pia alipokea madirisha ya aluminium na milango kwa ajili ya zahahanati ya Nandagala wilayani Ruangwa pamoja na kompyuta na  madftari kwa ajili ya shule za wilaya hiyo vyanye thamani ya sh.milioni 25 vilivyotolewa na Benki ya NMB. Makabidhiano hayo yalifanyika kwenye viwanja vya zahanati ya Nandagala
Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akitazama vifaa mbalimbali  vya hospitali vilivyotolewa na Taasisi ya Helping Hand  na Taasisi ya Jamii Bora kwa ajili ya Hospitali, Zahanati na Vituo vya Afya wilayani Ruangwa, kwenye viwanja vya Zahanati ya Nandagala wilayani humo, Julai 28, 2019. Makabidhiano ya vifaa hivyo yalifanyika kwenye Zahanati ya Nandagala. Wa pili kulia ni Mwenyekiti wa Taasisi ya Jamii Bora, Yassir Salim. 



Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akitazama vifaa mbalimbali  vya hospitali vilivyotolewa na Taasisi ya Helping Hand  na Taasisi ya Jamii Bora kwa ajili ya Hospitali, Zahanati na Vituo vya Afya wilayani Ruangwa, kwenye viwanja vya Zahanati ya Nandagala wilayani humo, Julai 28, 2019. Makabidhiano ya vifaa hivyo yalifanyika kwenye Zahanati ya Nandagala. Wa pili kulia ni Mwenyekiti wa Taasisi ya Jamii Bora, Yassir Salim. 
(Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu)

WAZIRI MKUU Kassim Majaliwa amepokea msaada wa vifaa tiba wenye thamani ya sh. milioni 250 vilivyotolewa na Shirika la Helping Hand for Relief and Development (HHRD) kwa Halmashauri ya Wilaya ya Ruangwa.

Baadhi ya vifaa hivyo ni vitanda vya kujifungulia, vitanda na magodoro ya wagonjwa, mashine za matibabu, viti vya wagonjwa (wheelchairs), vifaa vya maabara, mashine ya oksijeni, meza za kufanyia upasuaji, mablanketi, mafriji na samani za ofisini.

Akipokea msaada huo leo mchana (Jumapili, Julai 28, 2019) kwenye zahanati ya Nandagala, wilayani Ruangwa mkoani Lindi, Waziri Mkuu amewashukuru viongozi wa shirika hilo kwa kuchangia vifaa vingi ambavyo amesema vitasambazwa katika wilaya nzima ya Ruangwa.

“Tunawashukuru wadau wetu wa HHRD ambao wanashirikiana na taasisi ya Jamii Bora. Vifaa hivi ni kwa niaba ya wilaya nzima. Nitamkabidhi Mkuu wa Wilaya ili aone ni wapi pana uhitaji zaidi, naye atavisambaza,” amesema.

Akizungumza na wakazi wa kijiji cha Nandagala mara baada ya kupokea vifaa hivyo, Waziri Mkuu ambaye ni mbunge wa jimbo la Ruangwa, amesema ujenzi wa vituo vya afya kwenye kata za Mandawa, Nkowe na Mbekenyera umesaidia kuwafanya wananchi wa kata hizo wapate huduma muhimu za matibabu wakiwa huko huko.

“Kwenye bajeti ya mwaka huu, tunatarajia kupata sh. milioni 400 ambazo zitapelekwa Luchengelwa ili wapate kituo cha afya na huduma nyingine zote ziishie huko huko. Nimefurahi kumsikia Mkuu wa Wilaya akisema kuwa wataipigia debe zahanati ya Nandagala ili ipandishwe hadhi na kuwa kituo cha afya.”

Pia alilipongeza Shirika la HHRD kwa kuamua kuwahudumia watoto yatima, wajane na kuamua kutoa huduma za maji kwa kuchimba visima. “Ninawapongeza pia kwa kuamua kuwafundisha vijana wanaohitimu vyuo vikuu na kuwapa elimu ya ujasiriamali vijana wetu, kwa kuwaandaa wawe wabunifu na wajiajiri. Asanteni sana kwa kuwaondolea dhana ya ajira kwamba ni lazima washike kalamu na wakae ofisini,” alisema.

Mapema, akitoa taarifa ya msaada huo, Mwenyekiti wa Bodi ya HHRD, Bw. Yassir Salim Awadh alisema wana mradi wa utoaji vifaa tiba, chakula, nguo na sabuni unaolenga kuziwezesha hospitali za wilaya, mkoa na rufaa za Serikali, familia maskini na magereza ambao ulianza tangu mwaka 2014.

“Kupitia mradi huu, kati ya mwaka 2014 na 2018 tumeweza kugawa makontena 62 kwa nchi nzima. Mwaka huu 2019, tumepanga kuleta makontena 20 ambapo saba tayari yameshatumwa, matatu yameshafika na kugawiwa Zanzibar, manne yako njiani na yanatarajiwa kufika Oktoba, 2019.”

Alisema thamani ya vifaa kwa makontena yote pamoja na yale yanayotarajiwa kufika mwaka huu ni sh. bilioni 23.75. “Kupitia mradi huu tumeweza kutoa vifaa tiba vya aina mbalimbali katika hospitali za Kivunge, Makunduchi, Mnazi Mmoja, Wete, Abdallah Mzee (zote za Zanzibar). Nyingine ni Temeke, Kisarawe, Muhimbili, Mwananyamala, Bagamoyo na leo ni katika wilaya ya Ruangwa,” alisema.

Pia alisema shirika hilo lenye makao yake makuu Marekani na linajishughulisha na utatuzi wa changamoto za kijamii kweye sekta za afya, elimu, mayatima na matukio ya dharura, limeweza kuhudumia watoto yatima waishio majumbani 250 kutoka shule tisa za wilayani Kisarawe kwa kuwapatia vifaa vya shule, upimaji wa afya, mafunzo ya kujitegemea, michezo na safari za kimasomo.

“Shirika pia linajihusisha na uchimbaji visima vifupi. Hadi mwaka huu tumechimba visima zaidi ya 100 katika wilaya za Mkuranga, Kilwa, Kigambini, Ilala, Temeke, Morogoro, Kilosa, na wilaya zote za Unguja.”

Bw. Awadh alisema huduma nyingine wanayotoa ni upasuaji wa mtoto wa jicho ambapo katika kipindi cha miaka mitatu wameweza kufanya operesheni 525 kwenye maeneo mbalimbali ikiwemo Kilwa, Kibaha, Mkuranga, Kisarawe, Unguja na Pemba. “Mwaka huu, tunatarajia kufanya operesheni nyingine 75 mkoani Dar es Salaam,” alisema.

Naye Mkazi wa Nandagala ‘A’, Bi. Atiya Chilatu aliishukuru taasisi ya HHRD kwa kuwapatia vifaa tiba kwenye zahanati yao. “Hii maana yake tutapata huduma zote hapahapa, hatuna haja ya kwenda wilayani,” alisema.

Kwa upande wake, Mkuu wa Wilaya ya Ruangwa, Bw. Hashim Mgandilwa alisema msaada wa vifaa hivyo utaharakisha ujenzi wa zahanati ya Nandagala. “Msaada huu utaharakisha safari ya kupandisha hadhi zahanati ya Nandagala ifikie kuwa kituo cha afya,” alisema.

Alisema wilaya hiyo imepokea sh. bilioni 1.5 kwa ajili ya ujenzi wa hospitali ya wilaya na kukiri kuwa wamepokea fedha nyingine za uboreshaji wa vituo vya afya katika kata za Mkowe, Mbekenyera na Mandawa. “Hadhi ya vituo hivi kwa sasa imebadilika,” alisema.
  
IMETOLEWA NA:
OFISI YA WAZIRI MKUU,        
JUMAPILI, JULAI 28, 2019.

No comments:

Post a Comment

ZanziNews Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.