Habari za Punde

Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Mhe.Dk. Ali Mohamed Shein Azungumza na Uongozi wa Wizara ya Elimu na Mafunzo ya Amali Zanzibar.

Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Mhe. Dk. Ali Mohamed Shein akizungumza na Uongozi wa Wizara ya Elimu na Mafunzo ya Amali Zanzibar, katika mkutano wa Utekelezaji wa Bajeti na Mpango Kazi wa Wizara hiyo kwa mwezi wa Julai 2018 hadi Juni 2019, uliofanyika ukumbi wa Ikulu Zanzibar. 
KATIBU Mkuu Kiongozi na Katibu wa Baraza la Mapinduzi Dk. Abdulhamid Yahya Mzee , Waziri wa Elimu na Mafunzo ya Amali Zanzibar Mhe. Riziki Pembe Juma na Mshauri wa Rais Pemba Dk. Maua Abeid Daftari wakiwa katika ukumbi wa mkutano na kushoto Katibu Mkuu Wizara ya Elimu na Mafunzo ya Amali Zanzibar Dk. Idrissa Muslim Hija, wakimsikiliza Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Mhe.Dk. Ali Mohamed Shein, akizungumza wakati wa mkutano huo wa Utekelezaji Bajeti na Mpango Kazi  wa Wizara hiyo kuazia mwezi wa Julai 2018 hadi Juni 2019. 
Waziri wa Elimu na Mafunzo ya Amali Zanzibar Mhe. Riziki Pembe Juma akiwasirisha ripoti ya Utekelezaji wa Bajeti na Mpango Kazi wa Wizara hiyo kuazia mwezi wa Julai 2018 hadi Juni 2019, uliofanyika katika ukumbi wa Ikulu Zanzibar.
Katibu Mkuu Wizara ya Elimu na Mafunzo ya Amali Zanzibar Dk. Idrissa Muslim Hija akisoma taarifa ya Utekelezaji wa Bajeti na Mpango Kazi wa Wizara yake wakati wa mkutano huo na Rais wa Zanzibar Mhe.Dk. Shein uliofanyika ukumbi wa Ikulu Zanzibar.




No comments:

Post a Comment

ZanziNews Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.