Habari za Punde

ZBS Yakabidhi Fedha Kwa Ajili ya Umaliziaji wa Kituo Cha Afya

AFISA mdhamini wizara ya Biashara na Viwanda Pemba, Ali Suleiman  Abeid (wanne kutoka kulia)  akimkabidhi Katibu wa Jumuiya ya maendeleo jimbo la Konde Ismail Ali Juma,  Shilingi million 4,000,000/= zilizotolewa na Taasisi ya Viwango Zanzibar (ZBS) kwa lengo la kusaidia Kukamilisha mahitaji ya kituo cha Afya Cha Ungi Msuka Wilaya ya Wete Mkoa wa Kaskazn Pemba.
MRAJIS wa Jumuiya zisizoza kiserikali Zanzibar Ahmed Khalid Abdalla, akizungumza katika mkutano wa makatibu Tawala Mkoa na Wilaya, wakurugenzi wasaidizi Mktambuka wa Mabaraza ya Miji na Masheha, juu ya usimamizi wa NGOs Pemba
MKUU wa Mkoa wa Kusini Pemba Hemed Suleiman Abdalla, akifungua semina ya siku moja kwa masheha, makatibu Tawala Mkoa na Wilaya, wasaidizi wakurugenzi Mtambuka wa mabaraza ya Miji, juu ya usimamiaji wa NGOs Pemba.


BAADHI ya Masheha na watendaji kutoka mabaraza ya miji na Halmashauri Pemba, wakifuatilia kwa makini uwasilishwaji wa mada mbali mbali, wakati wasemina ya kuwajengea uwelewa juu ya usimamiaji wa NGOs Pemba.
(PICHA NA ABDI SULEIMAN, PEMBA)

No comments:

Post a Comment

ZanziNews Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.