Habari za Punde

Madaktari Wanafunzi Tanzania kukutana Zanzibar


MWENYEKITI  waBaraza la VijanaTaifa Zanzibar KhamisKheri (Wa pili kulia), akielezeaumuhimuwamkutanowa Chama cha MadaktariWanafunzi Tanzania (TAMSA) wanaosomakatikavyuovikuumbalimbalinchini, unaotarajiwakuanzakeshoOktoba 19, 2019 visiwani Zanzibar. KuliakwakeniMwenyekitiwa TAMSA Mohammed Hassan, akifuatiwanaMwenyekitiwakamatiyamaandaliziyamkutanohuo, Dkt. Yahya Simba.

Na SalumVuai
MKUTANO Mkuu wa Chama cha Madaktari Wanafunzi Tanzania (TAMSA), unatarajiwa kufanyika Jijini Zanzibar kuanzia kesho Oktoba 19 hadi 21, 2019 ukijumuisha zaidi ya washiriki 260 kutoka Vyuo Vikuu mbali mbali vya afya kote nchini.

Akizungumza leo na waandishi wa habari katika ukumbi wa Jumuiya ya Watu Wasioona Zanzibar (ZANAB), Mwenyekiti wa chama hicho Mohammed Hassan Mohammed, amesema mkutano huo wa kumi utatanguliwa na maonesho ya huduma za upimaji afya bila ya malipo.

Alisema maonesho hayo yamepangwa kufanyika katika eneo la Mapinduzi Square Michezani mjini Zanzibar, ambapo zaidi ya watu 3000 wanatarajiwa kufanyiwa uchunguzi wa kiafya pamoja na kupatiwa matibabu yatakayotolewa kiwanjani hapo.

Hassan alisema maonesho hayo yatapata baraka za kufunguliwa na Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar.Mhe.Balozi Seif Iddi atakayekuwa mgeni rasmin ambapo wanafunzi wa vyuo hivyo watatoa huduma kwa lengo la kusaidia jamii yenye mahitaji ya uchunguzi na matibabu, kabla ya kufungwa na Waziri wa Afya Zanzibar,Mhe. Hamad Rashid  Mohammed siku inayofuata.

Baada ya maonesho hayo kesho, Spika wa Baraza la Wawakilishi Zanzibar Mhe.Zubeir Ali Maulid, atafungua mkutano mkuu unaotarajiwa kufanyika Oktoba 21, 2019 katika jengo la ‘Abla Beach Apartments’ lililoko Beit El Ras Wilaya ya Magharibi ‘B’.

Pamoja na mambo mengine, mkutano huo utajadili na kutathmini mafanikio ya huduma za afya na changamoto zake nchini Tanzania, hasa ikizingatiwa kuwa TAMSA inaunga mkono juhudi za serikali zote mbili za Tanzania katika kuhakikisha wananchi wanapata huduma bora za afya mijini na vijijini.

Kwa upande wake, Mwenyekiti wa kamati ya maandalizi ya mkutano huo Dkt. Yahya Simba, alisema hiyo ni mara ya pili kufanya mkutano huo Zanzibar lengo wakiwa na vitu tafauti ilivyoviandaa yenyewe badala ya kuwashirikisha kwenye shughuli za taasisi nyengine.

Alisema kesho Oktoba 19, itakuwa fursa pekee kwa watu wenye ulemavu kufanyiwa uchunguzi wa kiafya, na Oktoba 20 kutatolewa elimu ya hedhi kwa wanafunzi wa kike ikiwa miongoni mwa ratiba ya maonesho hayo sambamba na huduma za ugonjwa wa saratani.

Aidha alifahamisha kuwa Oktoba 22, mwaka huu, kutafanyika kongamano kubwa la kisayansi ambapo zaidi ya maspika 15 kutoka Tanzania na nje wamealikiwa, ambapo kauli mbiu ni “Afya bora kwa wote”, ikichambua mafanikio na hatua ambazo Tanzania imefikia kwa upande huo.

Alisema sababu nyengine ya kufanyika mkutano huo hapa Zanzibar, ni mafanikio makubwa yaliyopatikana katika kutoa huduma bora za afya, akisema juhudi za serikali katika sekta hiyo zinaonekana wazi, huku akizitaja taasisi 17 zilizojitolea kuwaunga mkono ikiwemo wadhamini wakuu TIRA.

Mada mbali mbali zitawasilishwa kwenye mkutano mkuu ikiwemo kongamano la tafiti za kisayansi pamoja na elimu ya kujenga mawazo ya biashara na miradi yenye kukubalika kwa wawezeshaji na hatimaye kuleta tija kwa wahusika.

Mkutano huo utafikia tamati Oktoba 23, ambapo washiriki wote watapata fursa ya kufanya ziara katika mashamba ya viungo pamoja na maeneo mengine ya kihistoria, ikilenga kutangaza vivutio vya kitalii vilivyopo visiwani  Zanzibar.

IMETOLEWA NA IDARA YA HABARI MAELEZO
ZANZIBAR-18 OKTOBA, 2019

No comments:

Post a Comment

ZanziNews Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.