Habari za Punde

Waziri Mkuu Mhe. Kassim Majaliwa Amwakilishi Rais Dkt.Magufuli Katika Kutowa Tuzo Kwa Viwanda Vilivyofanya Vizuri 2018

Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa  akisalimiana na Waziri wa Nchi, Ofisi ya Waziri Mkuu  (Uwekezaji), Angela Kairuki wakati alipowasili kwenye hoteli ya Serena jijini Dar es salaam kumwakilisha Rais Dkt. John Pombe Magufuli  katika utoaji wa tuzo za Rais kwa viwanda vilivyofanya vizuri kwa mwaka 2018, Oktoba 17, 2019. Katikati ni Waziri wa Viwanda na Biashara, Innocent Bashungwa
Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akisalimiana na Mwenyekiti wa Shirikisho la Viwanda Tanzania(CTI), Subhash Patel wakati alipowasili kwenye hoteli ya Serena jijini Dar es salaam kumwakilisha Rais Dkt. John Pombe Magufuli  katika  utoaji wa tuzo za Rais kwa viwanda vilivyofanya vizuri kwa mwaka 2018, Oktoba 17, 2019. Katikati ni Waziri wa Nchi, Ofisi ya Waziri Mkuu (Uwezeshaji), Angela Kairuki. 
Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akizungumza wakati alipomwakilisha Rais, Dkt. John Pombe Magufuli katika utoaji wa tuzo za Rais kwa viwanda vilivyofanya vizuri kwa mwaka 2018 kwenye hoteli ya Serena jijini Dar es salaam
Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akimkabidhi tuzo ya ushindi wa jumla, Satbir Singh Hanspaul ambaye ni Mtendaji Mkuu wa Makampuni ya HANSPAUL wakati alipomwakilisha Rais, Dkt. John Pombe Magufuli katika utoaji wa tuzo za Rais kwa viwanda vilivyofanya vizuri kwa mwaka 2018 kwenye hoteli ya Serena jijini Dar es salaam, Oktoba 17, 2019. Watatu kushoto ni Waziri wa Viwanda na Biashara, Innocent Bashungwa na Kushoto ni Mwenyekiti wa  Shirikisho la Viwanda Tanzania (CTI), Subhash Pate.
Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akiwa katika picha ya pamoja na watoto Janainnah Salum (katikati), Fatma Khery (kushoto) na Rahma Hassani ambao aliomba kupiga nao picha baada ya kuvutiwa na sarakasi waliyoonyesha wakiwa na kikundi cha Safi cha Bungoni jijini Dar es salaam katika  utoaji wa tuzo za Rais kwa viwanda vilivyofanya vizuri kwa mwaka 2018 zilizofanyika kwenye hoteli ya Serena,  Oktoba 17, 2019. 
(Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu)

No comments:

Post a Comment

ZanziNews Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.