Mkurugenzi Mtendaji ,Wakala wa Usajili wa Matukio ya Kijamii Zanzibar Dkt.Hussein K. Shaaban akizungumza na waandishi wa habari wa vyombo mbali mbali kuhusu uzinduzi wa vitambulisho vipya ambavyo vitakuwa na "Chip" (Smart Cards) huko katika Ukumbi wa Wizara ya Habari Utalii na Mambo ya kale Kikwajuni.
Baadhi ya Waandishi pamoja na Maofisa wa Wakala wa Usajili na Matukio wakimsikiliza Mkurugenzi Mtendaji ,Wakala wa Usajili wa Matukio ya Kijamii Zanzibar Dkt.Hussein K.Shaaban (ambae hayupo pichani ) kuhusu uzinduzi wa vitambulisho vipya ambavyo vitakuwa na "Chip" (Smart Cards) huko katika Ukumbi wa Wizara ya Habari Utalii na Mambo ya kale Kikwajuni..
Picha na Khadija Khamis -Maelezo Zanzibar,
Na Miza Kona Maelezo Zanzibar
Wakala wa Usajili wa Matukio ya Kijamii Zanzibar kesho wanatarajiwa vitambulisho vipya vya Mzanzibar huko katika ukumbi wa Shekh Idrisa Abdulwakili Kikwajuni Zanzibar.
Akizungumza na waandishi wa habari huko katika ukumbi wa Wizara ya Habari na Mambo ya Kale Mkurugenzi Mtendaji Dr. Hussein Khamis Shaaban amesema vitambulisho vitaanza kutolewa kwa awamu tofauti kwa wananchi wote.
Uzinduzi huo wa utoaji wa vitambulisho vipya unatokana na kukamilika kwa zoezi zima la mfumo mpya wa usajili wa uimarishaji wa taarifa za vitambulisho ili kuwa na hadhi na ubora.
Amefahamisha kuwa vitambulisho hivyo ni vyenye ubora ambavyo vitatumika kwa matumizi mengi kutokana na uwezo wake wa kubeba program mbalimbali za smat card.
Akizitaja program hizo ni pamoja na kuwa taarifa mama za utambulisho na alama za kibayolojia, taarifa za leseni ya udereva, taarifa muhimu za huduma za kiafya pamoja na kutumika katika miamala ya kifedha.
Mkurugenzi huyo alifafanua kwamba vitambusho hivyo vitatumika katika program hizo pale mtumiaji atakapopoteza moja ya kitambulisho chake anachotumia kwa kufuata sheria zilizowekwa.
Aidha amewasisitiza wananchi kuvienzi na kuvitunza vitambulisho hivyo kutokana na ubora wake ili kuepuka usumbufu na gharama zaidi kwa kuleta maendeleo nchini.
Uzinduzi huo utafanyika kesho saa 3.00 asubuhi Mgeni Rasmi anatarajiwa kuwa Rais wa Zanzibar Dr. Ali Mohamed Shein.
No comments:
Post a Comment