Habari za Punde

Waziri wa Afya Zanzibar Mhe.Hamad Rashid Azungumza na Waandishi wa Habari Kuhusiana Daktari Aliyeomba Rushwa.

Na Rahma Khamis Maelezo Zanzibar.
Waziri wa Afya Zanzibar, Hamad Rashid Mohammed amewataka wagonjwa kutoa taaarifa  wanapofikwa na jambo la udhalilishaji.
Ameyasema hayo huko Ofisini kwake Wizara ya afya, wakati akitoa akizungumza na waandishi wa habari kuhusiana na taarifa ya daktari wa Hospitali ya Chake kutaka rushwa ya ngono kwa mgonjwa.
Amesema kitendo hicho sio kizuri kwa taifa kwani kinawafanya wagonjwa kuwa  na wasiwasi ambao wanapohitaji matibabu wakati wanapofika hospitali.
Aidha amesema Serikali haikufurahishwa na kitendo  hicho hivyo kwa kushirikina na Wizara ya Afya wamechukua hatua  ya kumtaka muhusika kutoa taarifa ili hatua za kisheria zichukuliwe dhidi yake.
Pia Mhe. Hamad amesema katika kupambana na tatizo hilo Serikali imeamua kumsimamisha kazi daktari huyo ili kupitisha uchunguzi na kuchukua hatua za sheria ikiwa atathibitishwa kufanya udhalilishaji huo .
Hata hivyo Waziri huyo amewataka akina baba kushirikiana na wake zao wakati wanapokwenda Hospitali kimatibabu ili kuepuka vitendo vya udhalilishaji .
Akizungumzia suala la mshahara kuhusu daktari huyo Mkurugenzi Mtendaji Utumishi Wizara ya afya Ramadhan Khamis Juma amesema kwa sasa analipwa nusu mshahara hadi kukamilika uchunguzi na ikigundulika kufanya hivyo atasimamishiwa mshahara wake.
IMETOLEWA NA HABARI MAELEZO

No comments:

Post a Comment

ZanziNews Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.