Habari za Punde

Mkurugenzi Azungumza na Waandishi wa Habari Kuhusu Usafi wa Mji wa Zanzibar

Na Idara ya Habari (MAELEZO) Maelezo Zanzibar.    

Baraza la Manispaa limesema litaendelea na juhudi za kuhakikisha suala la usafi linaimarika katika maeneo ya mji wa Zanzibar ili kuona mji unakuwa katika mandhari ya kuvutia.
Akizungumza na Waandishi wa Habari  huko ofisi kwake  Malindi Mkurugenzi wa Baraza  hilo Said Juma Ahmada amesema juhudi hizo ni pamoja na kuongeza vikosi kazi maeneo mbalimbali ikiwemo katika maeneo ya masoko na barabara ili kuondoa tatizo la kuenea kwa taka ovyo.
Aidha ameitaka jamii kubadilika kwa kuacha na tabia ya kutupa taka bila ya kufuata utaratibu ili lengo la kuimarisha mazingira katika  Mji wa Zanzibar liweze kufikiwa na kuleta mafanikio.
Pamoja na Hayo Mkurugenzi huyo aliwataka wazazi na walezi kwenda kuwaandisha watoto wenye umri wa kuandikishwa ili kupata elimu iliyo bora
Aidha amesema kuwa kutompeleka mtoto skuli ni kumnyima haki yake ya msingi kwani suala la elimu Serikali ya Mapinduzi Zanzibar limeipa kipa umbele katika  kuona watoto wanapatiwa elimu.
Nae Mkurugenzi Afya na Mazingira kutoka Baraza la Manispaa Mjini Bwana  Ramadhan Kibabu Suleiman amesema kuwa suala la Afya Baraza hilo wameongeza muda wa saa 24 ya utoaji wa huduma kwa wazazi  katika vituo vya afya vya Mpendae,Sebleni na Chumbuni ili kuwaondoshea usumbufu wajawazito  wanapotaka kupatiwa huduma.

No comments:

Post a Comment

ZanziNews Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.