Habari za Punde

Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Mhe.Balozi Seif Ali Iddi Aifariji Familia ya Msanii Maarufu Zanzibar Mareheme Makame Faki (Sauti ya Zege)

 Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Balozi Seif Ali Iddi akiifariji Familia ya Gwiji wa Muziki wa Taarab Asilia na Kidumbaku Marehemu Makame Faki aliyezikwa Kijijini kwao Gamba Nyumba ya Nyasi Mkoa wa Kaskazini Unguja.Msanii Makame Faki alifariki Dunia jana katikam Hospitali ya Global alikokuwa akipata huduma za Matibabu baada ya kusumbuliwa na Tumbo hapo majuzi.
Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Balozi Seif Ali Iddi akiifariji Familia ya Gwiji wa Muziki wa Taarab Asilia na Kidumbaku Marehemu Makame Faki aliyezikwa Kijijini kwao Gamba Nyumba ya Nyasi Mkoa wa Kaskazini Unguja.Msanii Makame Faki alifariki Dunia jana katikam Hospitali ya Global alikokuwa akipata huduma za Matibabu baada ya kusumbuliwa na Tumbo hapo majuzi.
Picha na – OMPR – ZNZ.
Na.Othman Khamis.OMPR.
Makamu wa Pili wa Rais w Zanzibar Balozi Seif Ali Iddi alisema Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar itaendelea kuthamini na kuunga mkono mchango unaotolewa na Wasanii Nchini katika harakati za Maendeleo kupitia Sekta ya Utamaduni.
Alisema Wasanii wamekuwa na mchango mkubwa katika masuala ya kuimarisha Uchumi hasa kwenye Sekta ya Utalii, Utamaduni na Kijamii ambapo Wadau hao hutumia vipaji vyao katika kupelekea Ujumbe kwa Jamii unaopelekea kuhamasisha njia za kuimarisha Uchumi huo.
Balozi Seif Ali Iddi alitoa kauli hiyo wakati akiifariji na kuipa pole Familia ya Msanii Mkongwe wa Muziki wa Taarab Asilia Visiwani Zanzibar Mzee Makame Faki aliyefariki Dunia na kuzikwa Kijijini kwao Gamba Nyumba ya Nyasi Mkoa wa Kaskazini Unaguja.
Alisema Marehemu Makame Faki akiwa Mmoja wa Wasanii wakubwa waliotoa mchango mkubwa katika Tasnia ya Taarabu hasa kike Kikundi chake cha Dumbaku ataendelea kukumbukwa na Taifa kwa ujasiri wake uliomuwezesha kupata fursa ya kutoa burdani ndani na nje ya Nchi.
Balozi Seif  aliiomba Familia ya Marehemu Makame Faki kuwa na subra katika kipindi hichi kigumu cha Msiba wa Kuondokewa na Mwanafamilia wao lakini ni vyema wakakumbuka kwamba Msiba huo sio wao pekee bali pia umeikumba Serikali na Taifa kwa Ujumla.
Akipokea pole hiyo kwa niaba ya Wanafamilia ya Msanii huyo, Mmoja wa Watoto wake Mtumwa Makame Faki aliishukuru Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar kutokana na moyo iliyoionyesha Familia hiyo wakati huu wa Msiba wa kuondokewa na Kipenzi chao.
Alisema yeye kwa niaba ya Wanafamilia hao wako pamoja na Swerikali yao katika masuala yote yanayoihusu Jamii na Wananchi wote wa Visiwa hivi pamoja na Tanzania kwa ujumla.
Marehemu Msanii Makame Faki aliyekuwa akipata huduma katika Hospitali ya Global baada ya kuzumbuliwa na Tumbo katika kipindi kifupi ameacha Vizuka Watatu na Watoto Tisa.
Wakati sisi tukiwa Marehemu watarajiwa, Mwenyenyezi Muungu  amjaalie Marehemu Makame Faki malazi mema Peponi. Amin.

No comments:

Post a Comment

ZanziNews Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.