Habari za Punde

Shamrashamra za Sherehe za Kuadhimisha Miaka 56 ya Mapinduzi ya Zanzibar Uzinduzi wa Jengo la Skuli ya Biashara Mombasa Zanzibar.

Muonekano wa Jengo Jipya la Skuli ya Biashara Mombasa Zanzibar lililojengwa na Mfanyabiasha na Mwakilishi wa Kuteuliwa Mhe. Ahmada Yahya Abdulwakil na kushirikiana na SMZ katika kumaliza ujenzi huo na kukamilika kwakwe. Ili kutowa Elimu ya Masomo ya Biashara kwa Wanafunzi wataochagulia. 
Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Mhe.Dk. Ali Mohamed Shein akisalimiana na Mfanyabiashara na Mwakilishi wa kuteuliwa Mhe. Ahmada Yahya Abdulwakil aliyejengo Skuli hiyo na kushoto Spika wa Baraza la Wawakilishi Zanzibar Mhe.Zuberi Ali Maulid na kulia Mkuu wa Mkoa wa Mjini Magharibi Unguja Mhe.,Hassan Khatib Hassan, alipowasili katika viwanja vya Skuli hiyo kwa ajili ya ufunguzi iliwa ni shamrashamra za kuadhimisha Miaka 56 ya Mapinduzi ya Zanzibar.
Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Mhe.Dk. Ali Mohamed Shein akiwa Waziri wa Elimu na Mafunzo ya Amali Zanzibar.Mhe.Riziki Pembe Juma wakielekea katika eneo lililoandaliwa kwa ajili ya Ufunguzi wa Skuli hiyo.
Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Mhe.Dk. Ali Mohamed Shein akiondoa kipazia kuashiria kuifungua Skuli ya Biashara Mombasa Zanzibar (kulia kwa Rais) Mhe.Riziki Pembe Juma na (kushoto kwa Rais) Mfanyabiashara na Mwakilishi wa Kuteuliwa aliyejenga Skuli hiyo Mhe. Ahmada Yahya Abdulwakil, wakishiriki katika kuondoa kipazia kuashiria ufunguzi huo  uliofanyika jana katika jengo la hilo ikiwa ni shamrashamra za kuadhimisha miaka 56 ya Mapinduzi ya Zanzibar. 
Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Mhe.Dk. Ali Mohamed Shein akikata utepe kuashiria kuifungua Skuli ya Biashara Mombasa Zanzibar (kulia kwa Rais) Waziri wa Elimu na Mafunzo ya Amali Zanzibar.Mhe Riziki Pembe Juma na Katibu Mkuu wa Wizara hiyo Dkt.Idrisa Muslim Hija na (kushoto kwa Rais) Mfanyabiashara Mhe. Ahmada Yahya Abdulwakil wakishirika katika hafla hiyo ya ufunguzi wa Skuli hiyo, ikiwa ni shamrashamra za kusherehekea Maadhimisho ya Miaka 56 ya Mapinduzi ya Zanzibar.
No comments:

Post a Comment

ZanziNews Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.