Habari za Punde

Uongozi wa Wizara ya Biashara na Viwanda Yawasilisha Taarifa ya Utekelezaji wa Mpangio Kazi kwa Mwezi wa Julai Hadi Disemba 2019 /2020.

Waziri wa Biashara na Viwanda Zanzibar Mhe. Balozi Amina Salum Ali akiwasilisha muktasari wa Taarifa ya Utekelezaji wa Mpango Kazi kwa Wizara yake wakati wa mkutano huo uliofanyika katika Ukumbi wa Ikulu Jijini Zanzibar, kushoto Katibu Mkuu Kiongozi na Katibu wa Baraza  la Mapinduzi.Dkt. Abdulhamid Yahya Mzee.
Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Mhe.Dk. Ali Mohamed Shein, akiongoza Kikao cha  mkutano wa kuwasilisha Taarifa ya Utekelezaji wa Mpango Kazi kwa Wizara ya Biashara na Viwanda Zanzibar kwa kipindi cha mwezi wa Julai hadi Disemba 2019 / 2020, uliofanyika katika ukumbi wa Ikulu Jijini Zanzibar. 
Katibu Mkuu Wizara ya Biashara na Viwanda Zanzibar Ndg. Juma Hassan Reli akiwasilisha Taarifa ya Utekelezaji wa Wizara ya Biashara na Viwanda kwa  mwezi wa Julai hadi Disemba 2019 / 2020, uliofanyika katika ukumbi wa Ikulu Jijini Zanzibar, ukiongozwa na Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Mhe.Dk. Ali Mohamed Shein. (hayupo pichani) 
Naibu Waziri Wizara ya Biashara na Viwanda Zanzibar Mhe. Hassan Khamis Hafidh akizungumza wakati wa mkutano wa Utekelezaji wa Mpango Kazi kwa Wizara yake uliofanyika ukumbi wa Ikulu Jijini Zanzibar. 
BAADHI ya Maofisa wa Idara za Wizara ya Biashara na Viwanda Zanzibar wakifuatilia  uwasilishwaji wa Utekelezaji wa Mpango Kazi kwa mwezi wa Julai hadi Disemba 2019/2020, uliofanyika katika ukumbi wa Ikulu Jijini Zanzibar, wakati Katibu Mkuu wa Wizara ya Biashara na Viwanda Zanzibar.Ndg. Juma Hassan Reli akiwasilisha mpango kazi (hayupo pichani) 
BAADHI ya Maofisa wa Idara za Wizara ya Biashara na Viwanda Zanzibar wakifuatilia  uwasilishwaji wa Utekelezaji wa Mpango Kazi kwa mwezi wa Julai hadi Disemba 2019/2020, uliofanyika katika ukumbi wa Ikulu Jijini Zanzibar, wakati Katibu Mkuu wa Wizara ya Biashara na Viwanda Zanzibar.Ndg. Juma Hassan Reli akiwasilisha mpango kazi (hayupo pichani) 
MKURUGENZI Biashara Ndg. Khamis Ahmada Shauri akichangia wakati wa mkutano wa Utekelezaji wa Mpango Kazi kwa Kipindi cha cha mwezi Julai hadi Disemba 2019/2020, uliofanyika katika ukumbi wa Ikulun Jijini Zanzibar
AFISA  wa Idara ya Vipimo na Biashara Ndg. Mohammed Mwalim . akichangia wakati wa mkutano wa  Utekelezaji wa Mpango Kazi kwa kipindi cha mwezi wa Julai hadi Disemba 2019/2020, uliofanyika katika ukumbi wa Ikulu Jijini Zanzibar, ukiongozwa na Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Mhe.Dk. Ali Mohamed Shein, (hayupo pichani) 

No comments:

Post a Comment

ZanziNews Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.