Habari za Punde

Makatibu Wakuu Wastaaf wa CCM Wahojiwa

10 Februari, 2020 Dar es Salaam
Makatibu Wakuu Wastaafu wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) Ndg. Yusuf Makamba na Ndg. Abdulrahaman Kinana leo Februari 10, 2020 wamefika katika Ofisi Ndogo za CCM Lumumba Jijini Dar es Salaam kuitikia wito wa Kamati Ndogo ya Usalama na Maadili inayoongozwa na Ndg. Philip Mangula

Makatibu Wakuu hao Ndg. Abdulrahman Kinana na Ndg. Yusuf Makamba wamefika katika Ofisi hizo majira ya mchana na kupokelewa na Makamu Mwenyekiti wa CCM (Bara) Ndg. Philip Mangula na Katibu Mkuu wa CCM Ndg. Bashiru Ally Kakurwa.
Ndg. Abdulrahman Kinana akiwa ofisini kwa Makamu Mwenyekiti wa CCM Bara Ndg. Philip Mangula baada ya kuitikia wito wa kuhojiwa na Kamati Ndogo ya Usalama na Maadili ya CCM.

Katibu Mkuu wa CCM Ndg.Bashiru Ally Kakurwa akizungumza na kuagana na Mzee .Yusuf Makamba, baada ya kuitikia wito wa Kamati Ndogo ya Usalama na Maadili ya CCM.


Imetolewa na,
HUMPHREY POLEPOLE
KATIBU WA ITIKADI NA UENEZI
CHAMA CHA MAPINDUZI (CCM)

No comments:

Post a Comment

ZanziNews Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.