Habari za Punde

KAMATI YA BUNGE YA KUDUMU YA IPONGEZA WMA


MwenyekitiwaKamatiyaKudumuya Bunge yaViwanda, BiasharanaMazingira,Mhe. Suleiman Ahmed Saddiq (Mb) (katikati) nawajumbewenginewakimsikilizakwamakiniAfisaMtendajiMkuuwaWakalawaVipimo (WMA), LudovickManege (kushotoaliyevaakotijeusi) marabaadayakutembeleakisima cha kuchujiamajinamafutakatikakituo cha UpimajiwaMaloriyabebayoMafutanaDirazaMaji (WMA) Misugusugumkoani Pwani
MenejawaWakalawaVipimo, Alban KihuldakielezajambombeleyaWabungewakamatiyaKudumuya Bunge yaViwanda, BiasharanaMazingira (hawapopichani) marabaadayakuwasilikituocha UpimajiwaMaloriyabebayoMafutanaDirazaMaji (WMA) Misugusugumkoani Pwaniikiwanimwendelezowaziarayasiku 10 kamatihiyokutembeleaviwanda.
Mwenyekiti wa Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Viwanda, Biashara na Mazingira, Mhe. Suleiman Ahmed Saddiq (Mb) (katikati) akielezea jambo mara baada ya kutembelea kituo cha Upimaji wa Malori yabebayo Mafuta na Dira za Maji (WMA) Misugusugu mkoani Pwani, kulia kwake ni Afisa Mtendaji Mkuu wa Wakala wa Vipimo (WMA),Ndg. Ludovick Manege
                                 Picha na Idara ya Habari Maelezo Dar es Salaam.

Na Erick Msuya - MAELEZO
Kamati ya  Bunge ya kudumu ya Viwanda, Biashara na Mazingira imewapongeza kituo cha Upimaji wa Malori yabebayo Mafuta na Dira za Maji (WMA) Misugusugu mkoani Pwani kwa kutambua malengo ya Serikali kuelekea Uchumi wa Viwanda.

Akizungumza na Waandishi wa Habari mara baada ya ziara yakutembelea kituo hicho Mwenyekiti wa kamati ya Bunge ya kudumu ya Viwanda, Biashara na Mazingira Mhe. Suleiman Ahmed Saddiq(Mb) amewataka kuendelea kujituma kwa kufata sheria na taratibu za upimaji.

“kwa kweli niwapongeze sana WMA wamefanya kazi kubwa sana na wamejiweka kisasa zaidi kwenye kila eneo hususani kuelekea Tanzania ya Viwanda, na tumejionea changamoto nyingi tukiwa kule Dodoma, leo tumekuja kupata majibu… waendelee kufanyakazi” amesema Mhe. Saddiq (Mb)

Aidha alibainisha kuwa WMA imekuwa msaada mkubwa utatuzi wa changamoto za ubadhilifu wa mita za maji uliokuwa unafanywa na baadhi ya mamlaka husika katika lengo la kibiashara iliyosababisha kero kwa watumiaji wa mita hizo. 

“nimefurahi leo nimepata majibu sahihi ya tatizo la mita za maji, mita zote lazima kabla ya kwenda kwenye mamlaka husika mfano DAWASA,DUWASA, MURUWASA lazima zote zipitie hapa WMA na kuhakikiwa kisha kupewa kibari tayari kutumika kwenye jamii” amesema Mhe. Saddiq (Mb)

Naye Afisa Mtendaji Mkuu wa wakala wa Vipimo (WMA), Ludovick Manege, amesema mafanikio ya kituo hicho yametokana na kujituma na kupata ushirikiano mkubwa kutoka Serikalini kwa kutatua baadhi ya changamoto.

“tupo kwenye mwaka mmoja wa mafanikio ya kituo hiki kimejengwa kwa pesa za Serikali, huku ikiwa na dhama ya kuhakikisha mafuta yanasambazwa kwa vipimo sahihi na maji katika miradi mikubwa ya Serikali yanasambazwa kwa vipimo sahihi” amesema Ludovick

Aliongeza “sisi tumepewa dhamana ya kuhakikisha matenki ya mafuta yanahakikiwa hapa, yanapoenda kujaza mafuta,  na Dira za Maji zinazoletwa nchini zote lazima zipimwe ili kuhakikisha mamlaka za maji zinatumia mita sahihi” amesema Ludovick
Kamati ya bunge ya kudumu ya Viwanda, Biashara na Mazingira wapo kwenye ziara ya siku 10 kwa kutembelea miradi mbalimbali nchini kwa kuona changamoto na kuzichukua ili kwenda kujadiliwa bungeni.

No comments:

Post a Comment

ZanziNews Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.