Habari za Punde

KAMATI YA USIMAMIZI MAAFA KILOMBERO YATAKIWA KUFANYA TATHMINI YA ATHARI ZA MAAFA YA MAFURIKO


Mkurugenzi Idara ya Menejimenti ya maafa Ofisi ya Waziri Mkuu, Kanali Jimmy Matamwe akiongea na baadhi ya  waathirika wa mafuriko wa Kijiji cha Nyange waliohifadhiwa katika shule ya sekondari  Nyange, wilayani Kilombero

Kufuatia Kaya 250 katika kata ya Msolwa Stesheni katika kijiji cha Nyange Wilayani Kilombero kuathirika na athari za maafa ya  mafuriko. Kamati ya Usimamizi wa Maafa ya Wilaya hiyo imeelekezwa kufanya tathmini ya awali kwa kata ya Mbanane na Kichangani ambazo takribani watu 350 wameathiriika na maafa hayo yaliyosababishwa na mvua zinazoendelea kunyesha hapa nchini.

Akiongea mara baada ya kukagua athari za maafa katika kata hizo, wilayani Kilombero, Mkurugenzi Idara ya Menejimenti ya maafa Ofisi ya Waziri Mkuu, Kanali Jimmy Matamwe, amesema tathmini ya awali ya athari za maafa katika kata hizo hainabudi kufanyika kwa haraka ili kubaini hatua za kuchukua katika kukabiliana na maafa hayo.

“Kwa mujibu wa Sheria ya Usimamizi wa maafa Na. 7 ya mwaka 2015, inaainisha  majukumu ya  kamati za usimamizi wa Maafa kuanzia ngazi ya Kijiji hadi mkoa, ambapo kwa mujibu wa sheria hiyo, jukumu la msingi ni kutafuta rasilimali kwa ajili ya usimamizi wa maafa katika ngazi husika, pamoja na  Kuratibu na kusimamia shughuli za usimamizi wa maafa na operesheni za dharura ndani ya Kijiji  wilaya au mkoa. Hivyo kamati hii haina budi kutekeleza majukumu yake kwa mujibu wa sheria.”amesisitiza Kanali Matamwe.

Awali akieeleza hatua ambazo kamati ya Menejimenti Usimamizi wa Maafa ya Wilaya hiyo ilizo zichukua, Mkuu wa Wilaya ya Kilombero, Mhe. James Ihunyo, amefafanua kuwa hadi kufikia tarehe 20 Machi 2020, kamati hiyo ilikuwa imefanikiwa kuwaokoa watu 350 ambao wamehifadhiwa kwenye shule ya sekondari Nyange.

“Tunaishukuru serikali kupitia, Ofisi ya Waziri Mkuu, Idara ya uratibu wa shughuli za maafa  kwa miongozo, lakini pia na kufika kwa wakati katika kata zetu, tumefurahi na mmetuletea mablanketi ambayo naamini yatawasaidia waathirika wa maafa haya ambao tumewahifadhi hapa shuleni. Kwa sasa wapo wanaume 172 na wanawake 178 huku watoto ni 30 ambao tumewahifadhi” Ameeleza  Mhe. Ihunyo.

Kwa mujibu wa Taarifa ya Mamlaka ya Hali hewa iliyotolewa mwezi Februari mwaka huu imeeleza kuwa kutakuwa na mvua za juu ya wastani katika eneo kubwa la nchi kati ya mwezi Machi hadi mwezi Mei, mwak huu, ambapo mvu ahizo zilitarajiwa kuanza kati ya wiki ya kwanza au ya pili ya mwezi Machi na kutaraji akumaliziaka kati ya wiki ya kwanza au ya pili yamwezi Mei. Hivyo kutokana na mvua hizo wananchi hawanbudi kuchukua tahadhari za athari za mvua hizo. 
Mkurugenzi Idara ya Menejimenti ya maafa Ofisi ya Waziri Mkuu, Kanali Jimmy Matamwe akimkabidhi Mkuu wa Wilaya ya Kilombero, Mhe. James Ihunyo, mablanketi kwa ajili ya waathirika wa mafuriko wa Kijiji cha Nyange waliohifadhiwa katika shule ya sekondari Nyange, wilayani Kilombero.
Mkuu wa Wilaya ya Kilombero, Mhe. James Ihunyo, akiongea na baadhi ya  waathirika wa mafuriko wa Kijiji cha Nyange waliohifadhiwa katika shule ya Sekondari  Nyange, wilayani Kilombero 
 Baadhi ya vifaa vya nyumbani vya wakazi wa Kijiji cha Nyange vikiwa vimehifadhiwa kwenye shule ya sekondari Nyange,  baada ya kijiji hicho kupata atthari ya maafa ya mafuriko, kutokana na mvua zinazoendelea kunyesha maeneo mbalimbali hapa nchini.
Waokoaji wanaoratibiwa na Kamati ya Usimamizi wa Maafa ya Wilaya ya Kilombero, wakiwa katika kijiji cha Nyange, ili kuwaokoa wakazi wa kijiji hicho kilichozingirwa na maji, ambapo takribani watu 350 tayari wameokolewa kutoka kata ya Mbanane na Kichangani hadi kufikia Machi, 20, 2020. 
 Baadhi ya wakazi wa kijiji cha Nyange, wilayani Kilombero, wakitoa vifaa vyao kwenye makazi yao yaliyozingirwa na maji kutokana na athari ya maafa ya mafuriko. Jumla ya Kaya 250 zilizokuwa zimezingirwa na maji zimeokolewa na kuhifadhiwa shule ya sekondari Nyange.
Mkuu wa Wilaya ya Kilombero, Mhe. James Ihunyo, akimhakikishia Mkurugenzi Idara ya Menejimenti ya maafa Ofisi ya Waziri Mkuu, Kanali Jimmy Matamwe kufuatilia Kamati ya maafa kufanya tathmini ya awali ya athari za maafa katika kijiji cha Nyange Wilayani Kilombero wakati Mkurugenzi huo alipokutana na kamati hiyo 
Mkurugenzi Idara ya Menejimenti ya maafa Ofisi ya Waziri Mkuu, Kanali Jimmy Matamwe akimueleza  Mkuu wa Wilaya ya Kilombero, Mhe. James Ihunyo, umuhimu wa Kamati ya maafa kufanya tathmini ya awali ya athari za maafa katika kijiji cha Nyange Wilayani Kilombero wakati Mkurugenzi huo alipokutana na kamati hiyo.

Picha na Ibrahim Hamidu Afisa Habari Mwandamizi
Ofisi ya Waziri Mkuu.

No comments:

Post a Comment

ZanziNews Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.