Habari za Punde

SERIKALI YA MPANGO WA MAENDELEO WA TAIFA NA YA KIWANGO NA UKOMO WA BAJETI YA SERIKALI KWA MWAKA 2020/21

Waziri Mkuu, Mhe. Kassim Majaliwa akifungua kikao cha uwasilishwaji wa mapendekezo ya Serikali ya Mpango wa Maendeleo wa Taifa na ya Kiwango na ukomo wa Bajeti ya Serikali kwa mwaka 2020/21, uliofanywa na Waziri wa Fedha na Mipango, Mhe., bungeni Jijini Dodoma.
Waziri wa Fedha na Mipango, Mhe. Dkt. Philip Isdor Mpango (Mb) akiwasilisha bungeni mapendekezo ya Serikali ya Mpango wa Maendeleo wa Taifa na ya Kiwango na ukomo wa Bajeti ya Serikali kwa mwaka 2020/21, Dodoma, ambapo Serikali inatarajia kukusanya na kutumia jumla ya shilingi trilioni 34.88.
Katibu Mkuu Wizara ya Fedha na Mipango, Bw. Doto James (kushoto) akiteta jambo na Naibu wake, Bw. Adlof Ndunguru pamoja na Naibu Gavana wa Benki Kuu ya Tanzania, Dkt. Yamungu Kayandabila, muda mfupi kabla ya Waziri wa Fedha na Mipango, Mhe. Dkt. Philip Isdor Mpango (Mb) kuwasilisha mapendekezo ya Serikali ya Mpango wa Maendeleo wa Taifa na ya Kiwango na ukomo wa Bajeti ya Serikali kwa mwaka 2020/21, Dodoma.
Baadhi ya viongozi wa Wizara ya Fedha na Mipango wakifuatilia kwa umakini maelezo ya Waziri wa Fedha na Mipango, Mhe. Dkt. Philip Mpango kuhusu mapendekezo ya Serikali ya Mpango wa Maendeleo wa Taifa na ya Kiwango na ukomo wa Bajeti ya Serikali kwa mwaka 2020/21, Katika Ukumbi wa Msekwa, Jijini Dodoma.
Waziri wa Fedha na Mipango, Mhe. Dkt. Philip Isdor Mpango (kushoto) akiteta jambo na Waziri wa Kilimo, Mhe. Japhet Hasunga pamoja na Naibu Waziri wa Mifugo, Mhe. Abdallah Ulega muda mfupi kabla ya kuwasilisha mapendekezo ya Serikali  ya Mpango wa Maendeleo wa Taifa na ya Kiwango na ukomo wa Bajeti ya Serikali kwa mwaka 2020/21, katika ukumbi wa Msekwa, Jijini Dodoma.
Katibu Mkuu Wizara ya Fedha na Mipango, Bw. Doto James akiteta jambo na Naibu wake, Bw. Adolf Ndunguru, nje ya ukumbi wa Msekwa, mara baada ya kuwasilishwa kwa mapendekezo ya Serikali ya Mpango wa Maendeleo wa Taifa na ya Kiwango na ukomo wa Bajeti ya Serikali kwa mwaka 2020/21, bungeni Jijini Dodoma.(Picha na Farida Ramadhani-Wizara ya Fedha na Mipango-Dodoma)

No comments:

Post a Comment

ZanziNews Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.