Habari za Punde

Waziri wa Fedha na Mipango Zanzibar Mhe.Balozi Mohammed Ramia Atembelea Mradi wa Ujenzi wa Nyumba za Kwahani City Kuangalia Maendeleo ya Ujenzi Huo.

Waziri wa Fedha na Mipango Zanzibar Mhe. Balozi Mohammed Ramia akitembelea Mradi wa Nyumba za Kisasa za Kwahani City, alipofanya ziara kutembelea mradi huo katika mtaa wa kwahani Wilaya ya Mjini Unguja ,akiwa na Mshauri Elekezi wa Mradi huo Eng.Adrian Eradius kushoto kwa Waziri.Mradi huo unategemewa kumalizika kwa wakati uliopangwa kukamilika kwake.
Mshauri Elekezi wa Ujenzi wa Mradi wa Nyumba za Kwahani City Eng. Adrian Eradius, wa kwanza (kushoto) akitowa maelezo ya maendeleo ya ujenzi huo wakati wa ziara ya Waziri wa Fedha na Mipango Zanzibar Mhe.Balozi Mohammed Ramia, alipotembelea mradi huo. Mradi huo unatarajiwa kukamilika kwa wakati uliopangwa. 
Baadhi ya majengo ya Nyumba za Mradi wa Kwahani City Zanzibar Wilaya ya Mjini Unguja ukiendelea na ujenzi huo na kufikia hatua kubwa.

Waziri wa Fedha na Mipango Zanzibar Mhe. Balozi Mohammed Ramia akitembelea Mradi wa Nyumba za Kisasa za Kwahani City, alipofanya ziara kutembelea mradi huo katika mtaa wa kwahani Wilaya ya Mjini Unguja ,akiwa na Mshauri Elekezi wa Mradi huo Eng.Adrian Eradius kulia kwa Waziri.


No comments:

Post a Comment

ZanziNews Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.