Msajili
Msaidizi wa Vyama vya Siasa, Bw. Sisty Nyahoza akifafanua jambo mbele ya
viongozi wa Kitaifa wa Chama cha United Democratic Party (UDP) wakati wa zoezi
la uhakiki wa vyama vya siasa walipotembela Makao Makuu ya chama hicho leo
jijini Dar es Salaam. Katikati ni Mwenyekiti wa UDP Taifa, John Momose Cheyo.
Mhazini
wa Chama cha Wakulima (AAFP), Bw. Ndonge Said Ndonge akitoa maelezo kuhusu
namna wanavyo tunza taarifa zao za mapato namatumizi mbele ya Maafisa kutoka
Ofisi ya Msajili wa Vyama vya Siasa (ORPP) walipofika katika Ofisi za Makao
Makuu ya chama hicho kwa ajili ya zoezi la uhakiki lililoanza leo jijini Dar es
Salaam.
Maafisa Kutoka Ofisi ya Msajili wa
Vyama vya Siasa (ORPP) wakipitia nyaraka ya fedha za Chama cha Wakulima (AAFP) wakati
wa zoezi la uhakiki wa vyama vya siasa lililoanza leo jijini Dar es Salaam.
Kutoka kulia ni Kaimu Mkuu wa Idara ya Gharama za Uchaguzi na Ruzuku, Bi. Hollo
Kazi, Afisa Mipango wa Ofisi ya Msajili wa Vyama vya Siasa (ORPP), Bw. Emmanuel
na Mkaguzi wa Ndani Bw. Mussa Boma.
Mkuu
wa Idara ya Gharama za Uchaguzi na Ruzuku toka Ofisi ya Msajili wa Vyama vya
Siasa, Bi. Hollo Kazi akielezea jambo mbele ya viongozi wa Kitaifa wa Chama cha
Wakulima Tanzania (AAFP) wakati wa zoezi la uhakiki wa vyama vya siasa
walipotembela Makao Makuu ya chama hicho leo jijini Dar es Salaam. Kushoto ni
Afisa Mipango wa Ofisi ya Msajili wa Vyama vya Siasa (ORPP), Bw. Emmanuel
Msengi.
(Na:
Mpiga picha wetu)
No comments:
Post a Comment