Eneo hili la Kibandamaiti limezoeleka katika kipindi cha mvua za masika hujaa maji na Wananchi wa eneo hilo huhama kupisha kupita kwa mvua na kuondoka kwa maji yaliyojaa katika makazi yao.
Kwa sasa ni historia ya kujaa maji baada ya kukamilika kwa Mradi mkubwa wa ujenzi wa mitaro ya kupitishia maji katika maeneo sugu wakati wa kipindi kama hichi cha mvua za masika hujaa maji na Wananchi wake kuhama makazi yao kutokana kuingiliwa na maji majumbani mwao.
Kama inavyoonekana picha eneo hilo likiwa katika hali yake ya kawaida baada ya kumalizika kwa mvua ilionyesha jana na leo.
No comments:
Post a Comment