Habari za Punde

Wazazi Watakiwa Kushirikiana Kuzuiya Mikusanyiko ya Watoto Katika Baadhi ya Maeneo Kujikinga na Corona. Tutumize Wajibu Wetu Kupiga Vita Maambukizi ya Corona.

Na.Takdir Suweid -Zanzibar.
Mbunge wa Viti Maalum Faharia Shomari Khamis amewashauri Wazazi kushirikiana kuzuia Mikusanyiko ya Watoto katika baadhi ya maeneo ili kuwakinga na Corona.
Ameyasema hayo wakati alipokuwa akikabidhi Saruji kwa Viongozi wa Almad-rasatul-Khairia Islamia “B” iliopo Kilimahewa  Wilaya ya Mjini.
Akizungumza kwa niaba yake Mjumbe wa Kamati tekelezaji Umoja wa Wanawake (Uwt) Wilaya ya Mjini Asha Daudi amesema Serikali imefunga Skuli,Madrasa na kuzuia mikusanyiko ili kujikinga na Janga hilo.
Amesema baadhi ya Watoto katika Mitaa wanacheza Mpira wa Miguu,Gololi  na Michezo mengine jambo ambalo linahatarisha maisha yao.
Aidha amewaomba Wanajamii kutii agizo la Serikali la kuzuia mikusanyiko katika maeneo yao ili lengo la Serikali liweze kufanikiwa.
Kwa upande wake Mlezi wa Madrasa hiyo Sada Mwendwa amempongeza kiongozi huyo kwa kutekeleza ahadi yake ambapo amesema itasaidia kufanya matengenezo ili Wanafunzi wasome katika Mazingira mazuri wakati Madrsa zitakapofunguliwa.
Mbali na hayo amewaomba Wafadhili na Watu wenye Uwezo kuwasaidia kutatua matatizo yanayowakabili ikiwemo ukosefu wa Umeme na Maji.

No comments:

Post a Comment

ZanziNews Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.