Habari za Punde

Umoja wa Wazalenzo na Wafanyabiashara Katika Mapambano Dhidi ya Virusi vya Corona Wakabidhi Vifaa na Dawa Kwa Ajili ya Kinga Dhidi ya Corona Zanzibar.

Mwenyekiti wa Muungano wa Wafanyabiashara Wazalendo Kupambana na Maradhi ya Maambukizo ya Virusi vya Corona Tanzania. Ndg. Abdulsamad Abdulrahim akitowa maelezo kwa Waziri wa Nchi Ofisi ya Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar.Mhe Mohammed Aboud Mohammed mwenye kofia wakati wa hafla ya kukabidhi vifaa mbalimbali kwa ajili ya kujikinga na maambukizo ya Corona, vilivyotolewa na Umoja huo, makabidhiano hayo yamefanyika katika viwanja vya Ukumbi wa Sheikh Idrissa Abdulwakil Kikwajuni Jijini Zanzibar.

Waziri wa Nchi Ofisi ya Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Mhe. Mohammed Aboud Mohammed akiosha mikono wakati wa kupokea msaada wa vifaa mbalimbali likiwemo tanga hilo la maji kwa ajili ya kuosha mikoni vilivotolewa na Umoja wa Muungano wa Wafanyabiashara Wazalendo kwa ajili ya kupambana na virusi vya Corona. 
No comments:

Post a Comment

ZanziNews Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.