Habari za Punde

TANZIA: BABA MZAZI WA WAZIRI WA MAMABO YA NDANI YA NCHI, MHE. GEORGE BONIFACE SIMBACHAWENE AFARIKI DUNIA

Marehemu Boniface Simbachawene Mwataguluvala, baba mzazi wa Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, George Simbachawene, ambaye amefariki katika Hospitali ya Benjamini Mkapa, jijini Dodoma, leo.
Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, George Simbachawene (kushoto), akizungumza na Inspekta Jenerali wa Polisi (IGP), Simon Sirro, wakati Mkuu huyo wa Jeshi alipoenda kuhani msiba wa Baba Mzazi wa Waziri huyo, marehemu Boniface Simbachawene Mwataguluvala, Kinyerezi Jijini Dar es Salaam
Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, George Simbachawene (katikati), akimsikiliza Kamanda wa Polisi Mkoa wa Ilala, Zubery Chembera (kushoto), alipokuja kuhani msiba wa baba mzazi wa Waziri huyo, marehemu Boniface Simbachawene Mwataguluvala, Kinyerezi Jijini Dar es Salaam, leo Aprili 17, 2020. Kulia ni  Kamanda wa Polisi Kanda Maalum ya Dar es Salaam, SACP, Lazaro Mambosasa. 
Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, George Simbachawene (wapili kulia), akimsikiliza Inspekta Jenerali wa Polisi (IGP), Simon Sirro, wakati alipokuja kumfariji kwa kufiwa na baba yake Mzazi, marehemu Boniface Simbachawene Mwataguluvala, Kinyerezi Jijini Dar es Salaam
Inspekta Jenerali wa Polisi (IGP), Simon Sirro akisaini kitabu cha maombolezo ya kifo cha baba yake Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, George Simbachawene (aliyesimama), jijini Dar es Salaam, leo. Baba Mzazi wa Waziri huyo,  Boniface Simbachawene Mwataguluvala amefariki  katika Hospitali ya Benjamini Mkapa, jijini Dodoma, leo.
  Picha na Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi.
MHESHIMIWA GEORGE BONIFACE SIMBACHAWENE, WAZIRI WA MAMBO YA NDANI YA NCHI, ANASIKITIKA KUTANGAZA KIFO CHA BABA YAKE MZAZI, MZEE BONIFACE SIMBACHAWENE MWATAGULUVALA (91) KILICHOTOKEA LEO TAREHE 17 APRILI, 2020 SAA 9:45 ALFAJIRI KATIKA HOSPITALI YA BENJAMINI MKAPA JIJINI DODOMA.
HABARI ZIWAFIKIE:
1.      FAMILIA YA MAREHEMU WALIOKO KIJIJI CHA PWAGA, WILAYA YA MPWAPWA, MKOA WA DODOMA NA WALE WALIOKO NJE YA MKOA.
2.      VIONGOZI MBALIMBALI WA SERIKALI, VIONGOZI WA CHAMA CHA MAPINDUZI, NA VIONGOZI WA VYAMA VINGINE VYA SIASA.
3.      NDUGU, JAMAA NA MARAFIKI MBALIMBALI POPOTE PALE WALIPO.
MSIBA KWASASA UTAKUA SEHEMU ZIFUATAZO;
DAR ES SALAAM: NYUMBANI KWA MHE. WAZIRI, KINYEREZI.
DODOMA MJINI:    NYUMBANI KWA NDUGU SEMGURUKA/MAMA DEVY – ILAZO.
KIBAKWE:             NYUMBANI KWA MAREHEMU KIJIJI CHA PWAGA.
MWILI UTASAFIRISHWA KUTOKEA DODOMA MJINI SIKU YA JUMAPILI TAREHE 19/04/2020 BAADA YA IBADA FUPI ITAKAYOFANYIKA ILAZO. MAZISHI YATAFANYIKA TAREHE 20/04/2020, SIKU YA JUMATATU NYUMBANI KWA MAREHEMU, KIJIJI CHA PWAGA, JIMBO LA KIBAKWE, WILAYA YA MPWAPWA, MKOA WA DODOMA.
MWENYEZI MUNGU AILAZE ROHO YA MAREHEMU MAHALI PEMA PEPONI..AMINA

No comments:

Post a Comment

ZanziNews Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.