Habari za Punde

Atumikia Kifungo Cha Miaka 12 Kwa Kosa la Udhalilishaji

Na.Rahma Suleiman - Zanzibar.
Abuu Khamis Ibrahim (40) mkaazi wa Meya Mjini Zanzibar amehukumiwa kifungo cha miaka 12 jela kwa kosa la kubaka,kulawiti na kumtorosha Mtoto wa kike miaka 15 jina tunalihifadhi.

Mshtakiwa huyo amepewa adhabu hiyo na mahakama ya Mkoa Vuga mjini Zanzibar ambapo alitenda makosa hayo Febuari 24 mwaka jana 2019.

Akisomewa shtaka lake na hakimu wa mahakama hiyo Salum Hassan Bakari na Mwendesha Mashtaka Shamsi Yassin alieleza kuwa mshtakiwa huyo alimtorosha mtoto huyo ambae yupo chini ya uangalizi wa wazazi wake na kumfanyia udhalilishaki huo ambao ni kinyume na haki za binadamu.

"Febuari 24 mshtakiwa alimtorosha mtoto ambae yupo chini ya uangalizi wa wazazi wake na kuondoka nae majira ya saa kumi jioni na kumrejesha saa tatu usiku na kufanyia vitendo vya udhalioishaji kwa kumbaka na kumlawiti "alisema Hakimu Bakari Mahakamani hapo.

Alieleza kuwa mshtakiwa huyo amepewa adhabu ya kifungo cha miaka 12 jela na kutoa fidia ya Shilingi Milioni moja.

Kesi hiyo ilianzwa kusikilizwa Mahakamani hapo Julai 7 mwaka jana ambapo mahakama imejiridhisha na ushahidi uliotolewa mahakamani hapo.

No comments:

Post a Comment

ZanziNews Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.