Habari za Punde

Demokrasia Makini Walitaka Jiji la Zanzibar Kuimarisha Muindombinu ya Barabara.

Na.Takdir Swiweid -Maelezo.
Chama cha Demokrasia Makini kimeishauri Serikali kuweka mikakati ya kuzifanyia  matengenezo Barabara zilizomo katika Jiji la Zanzibar ili ziendane na hadhi ya Jiji hilo.
Akitoa Taarifa kwa vyombo vya habari huko Ofisini kwake Taveta Wilaya ya Magharibi ‘’B’’Unguja Katibu Mkuu wa Chama hicho Ameir Hassan Ameir amesema Barabara nyingi ni mbovu na haziridhishi hata kidogo hivyo zinaondosha haiba ya Jiji la Zanzibar.
Amesema babara zinazibwa Viraka mara kwa mara hivyo kufanyiwa matengenezo kutasaidia kupunguza gharama kwa Serikali na kunusuru maisha ya Watu na mali zao.
Aidha Katibu Ameir amesikitishwa na Watendaji wa UUB kuziba njia na kuchimbuka haraka kila inapofika msimu wa Mvua jambo ambalo linaisababishia hasara Serikali.
Hata hivyo amewashauri Watendaji hao kufanya kazi kwa ufanisi na kama wameshindwa kutoa fursa kwa wengine, watakaoweza kuleta mabadiliko na kunusuru matumizi mabaya fedha za Wananchi walipa kodi.

No comments:

Post a Comment

ZanziNews Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.