Habari za Punde

Mvua za Masika Zimeleta Madhara Katika Maeneo Mbalimbali Zanzibar Kwa Kujaa Maji

Wananchi wa maeneo ya Dunga Wilaya ya Kati Unguja wakivuka katika eneo la barabara jirani na Skuli ya Sekondari ya Dunga, barabara hiyo imejaa maji na kuchukuliwa hatua ya kuifunga kwa usalama wa Wananchi wanaotumia barabara hiyo kuelekea Dunga Mitini,Chwaka na Bambi, kwa sasa imefungwa kutoka na mvua za masaka zinazonyesha katika maeneo mbalimbali ya Zanzibar.    
Muonekano wa eneo la barabara ya Dunga ikiwa imefunikwa na maji kutokana na mvua za masika zinazoendelea kunyesha katika maeneo mbalimbali ya Zanzibar na kuleta madhara kwa baadhiu ya Wananchi nyumba zao kujaa maji na kuhama katika makaazi yao.
Wananchi wakivuka kutoka upande wa Dunga Mitii kuelekea upande wa pili kuelekea Mjini, barabara hiyo imebidi kuvungwa kwa kuhofia usalama wa watumiaji wa barabara hiyo kwa gari zinazoelekea shamba na kurudi mjini kutokana na kujaa kwa maji na kufunikwa barabara hiyo.
Kisima katika eneo la Dunga kikiwa kimevunikwa na maji kutokana mvua za masika zilizonyesha na kuleta majanga katika maeneo ya Wakazi hayo na kuhama. 
Mkaazi wa Dunga Wilaya ya Kati Unguja akiwa katika zoezi la kukosha baskeli yake katika eneo la barabara ya dunga iliyojaa maji ya mvua, kama alivyokutwa na Camera yetu  

No comments:

Post a Comment

ZanziNews Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.