Habari za Punde

Wananchi Watakiwa Kuva Barkoa Kupambana na Corona.

Na.Takdirn Suweid 
Mwakilishi wa Viti maalum Mhe.Mwanaidi Kassim Mussa amewakumbusha Wananchi kutodharau miongozi iliotolewa na Wataalamu wa Afya katika kupambana na Janga la Corona.
Amesema licha ya Serikali kulelegeza masharti kutokana na mafanikio makubwa ya kujikinga na Corona yaliopatikana  lakini baadhi ya Wananchi wanadharau jambo ambalo linaweza kusababisha Mripuko wa Maradhi hayo.
Akitoa taarifa kwa vyombo vya habari huko Kiembesamaki Wilaya ya Magharibi ‘’B’’amesema bado tahadhari kwa Wananchi zinahitaji kuchukuliwa kwa kuvaa Barakoa,kukosha mikono kwa sabuni na maji ya kutitika na kuondosha mikusanyiko isiyokuwa ya lazima ili kuzuia kurudi kwa kasi maambukizi ya Virusi vya Corona katika jamii.
Aidha ameipongeza Serikali kwa juhudi ilizozichukuwa katika kupambana na Covid 19 na kufanikiwa kurejesha masomo ya vyuo vikuu, kidato cha sita na ligi kuu ya Mpira wa Miguu.
  Hata hivyo ameiomba Wizara ya elimu na Mafunzo ya Amali na Wizara ya Vijana, Utamaduni, Sanaa na Michezo kukaa na Wizara ya Afya kutafuta mbinu zitakazo saidia Wanafunzi na Wanamichezo kubaki salama wakati harakati zikiendelea.
Mbali na hayo amewaomba Wazazi na Walezi kuwadhibiti watoto wao kuwacha mikusanyiko kama ya michezo jambo ambalo linaweza kuhatarisha Afya zao.

No comments:

Post a Comment

ZanziNews Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.