Na Jaala Makame Haji, ZEC
Tume
ya Uchaguzi ya Zanzibar ZEC imesema
itaendelea na utaratibu wa kuimarisha majengo ya ofisi za uchaguzi za
wilaya pamoja na kujenga majengo mapya ambayo yatasaidia wananchi kupata huduma
za kiuchaguzi katika maeneo ya karibu na makazi yao.
Mwenyekiti
wa Tume ya Uchaguzi ya Zanzibar Mhe.Jaji Mkuu Mstaafu Hamid Mahmoud Hamid ameyasema
hayo baada ya kuweka jiwe la msingi la ofisi ya uchaguzi ya wilaya ya Magharibi
“A” iliyopo Mwera Mkoa Mjini Magharibi.
Amesema,
Tume ya Uchaguzi inawajibu wa kuwa karibu na wananchi wake ili kufikia dhamira
ya ushiriki wa wananchi katika hatua zote za uchaguzi nchini.
Mkurugenzi wa Uchaguzi Thabit Idarous Faina amesema
kuwepo kwa jengo hilo kutarahisisha upatikanaji wa huduma kwa wananchi wa Magharibi
“A” hasa katika kipindi hiki cha kuelekea Uchaguzi Mkuu 2020.
Afisa Uchaguzi wa wilaya hiyo Suluhu Ali Rashid amewata
wananchi kuwa na utaratibu wa kuzitumia ofisi za uchaguzi za wilaya hatua
ambayo itasaidia upatikanaji wa taarifa sahihi.
Ujenzi
wa jengo la ofisi ya uchaguzi ya wilaya ya Magharib “A” unasimamiwa na fundi
dhamana mzalendo Mohamed Mkuta kutoka Kampuni Ya Trip Construction limited
iliyopo Kijito Upele Zanzibar
No comments:
Post a Comment