Habari za Punde

Mkuu wa Wilaya ya Kaskazini B Unguja

Mkuu wa Wilaya ya Kaskazini "B" Unguja Ndg. Rajab Ali amewataka wakulima wa bonde la Pangeni lililopo Wilaya Kaskazini B Unguja kufuata mbinu Bora za kilimo cha mpunga kinachokabiliana na mabadiliko ya tabia nchi wakati wa ziara yake kutembelea bonde hilo.
Ameyasema hayo huko Pangeni alipokua anazungumza na wakulima wa Wilaya hiyo wakati wa Maashimisho ya Siku ya Wakulima iliyoandaliwa na mradi wa kilimo himilivu uliofadhiliwa na USAID na kusimamiwa na IITA, FAO, USDA,World  Agroforestry Center ,Serikali ya Muungano na Serikali ya Zanzibar.

Nd, Rajab hakuacha kutoa masikitiko Yake Kwa wakulima Kwa kupatiwa mafunzo mara Kwa mara lakini ukienda kutembelea mashamba ya yanakua katika Hali mbaya. 

Rajab ametoa shukrani zake Kwa wafadhili wa mradi huo, pia alipata nafasi ya kutembelea mashamba ya mfano katika bonde hiloNo comments:

Post a Comment

ZanziNews Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.