Waziri wa Nchi Ofisi
ya Rais, Utumishi wa Umma na Utawala Bora wa Zanzibari, Mhe.Haroun Ali Suleiman
(wa kwanza kulia), akizungumza katika Kikao kifupi na Tume ya Haki za Binadamu
na Utawala B ora walipomtembelea Ofisini kwake Mjini Unguja, Zanzibari Juni 4,
2020, kulia ni Mwenyekiti wa Tume hiyo Jaji Mstaafu Mathew Mwaimu, Makamu
Mwenyekiti Mohamedi Khamis Hamadi, na kushoto ni watendaji kutoka Ofisi ya
Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais, Utumishi wa Umma na Utawala Bora.
Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais, Utumishi wa Umma
na Utawala Bora wa Zanzibari, Mhe.Haroun Ali Suleiman akiwa kwenye picha ya
pamoja na ujumbe wa Tume ya Haki za Binadamu na Utawala Bora, na
watendaji kutoka Wizara yake mara baada ya mazungumzo mafupi kuhusu masuala ya
haki za binadamu na utawala bora,ujumbe huo
ulimtebelea ofisini kwake Mjini Unguja Zanzibari
Na.Mwandishi
Wetu- MAELEZO
Waziri wa Nchi Ofisi
ya Rais, Utumishi wa Umma na Utawala Bora wa Zanzibari, Mhe.Haroun Ali Suleiman
amesema kuwa Serikali inatakeleza jukumu kubwa la kuwapatia wananchi huduma mbalimbali
na kukidhi tafsiri halisi ya utawala bora katika kutekeleza kazi zake.
Akizungumza Ofisini
kwake Mjini Unguja, Zanzibari alipotembelewa na ujumbe wa Tume ya Haki za
Binadamu na Utawala Bora amesema kuwa moja ya ishara ya utawala bora katika
nchi yeyote duniani ni pamoja na kuheshimu haki za binadamu kwa sababu ni
msingi mkubwa katika kutekeleza majukumu ya Serikali kwa kila mwananchi.
“Haki za binadamu
limekuwa ni jambo lenye mjadala kila kona kwa sababu kila jambo linalotendeka
liwe zuri au baya ni haki za binadamu, hasahasa jambo likiwa baya utaambiwa
umevunja haki za binadamu, Serikali yetu inatimiza jukumu kubwa la kulinda haki
za binadamu kwa kila mwananchi na huo ndiyo utawala bora”, Alisema Waziri
Suleiman
Alisema kuwa katika
utawala bora Serikali imejenga nidhamu kubwa ya kazi kwa watumishi wote wa umma
na imetenga siku ya utawala bora ambayo imeingizwa kwenye siku ya maadili na
hapa Serikali inajitathmini kwa mwaka mmoja kipi ambacho imefanikiwa na kipi
ambacho hajafanikiwa.
Aidha, Waziri alisema
kuwa katika utekelezaji wamasuala ya Utawala bora kwasasa hali ni tofauti na
zamani kwani kila mwananchi anapatiwa huduma ya haki kwa kutumia kitengo cha
Idara ya Msaada wa Sheria kilichopo Wizara ya Sheria na Katiba ambacho kimekuwa
msaada mkubwa kwa kila mwananchi wa Zanzibari.
“Mambo ya utawala
bora hapa Zanzibari yalianza zamani wakati wa Rais wa Kwanza wa Zanzibari
Hayati Abeid Karume alipoanzisha Wizara
ya kuweka hali za wananchi sawa nah ii ilikuwa na madhumi makubwa kwani
ilizingatia haki za binadamu kwa upana zaidi”, alisema Waziri Suleiman
Alibainisha kuwa Tume
ina jukumu kubwa la kusimamia haki za binadamu kwa Serikali ya Jamhuri ya
Muungano wa Tanzania hususani kusimamia tafsiri halisi ya neno haki za
binadamu, aliongeza kuwa kwenye utawala
bora Serikali yetu ya Tanzania umetimiza kwa kiasi kikubwa hasa kuleta
maendeleo Makubwa na nidhamu kazini.
Utawala bora ? Please tuache utani, kila mzanzibar apewe kipande chake cha uzanzibar ili waweze kujiandikisha kwenye book la wapiga kura, huo ndio utawala bora
ReplyDelete