Habari za Punde

Wakulima wa mwani Kusini Unguja wkabiodhiwa msaada wa vihori ikiwa ni ahadi ya Serikali kuwasiaida wakulima hao

 WAKULIMA wa mwani Mkoa wa Kusini Unguja, wakiwa katika vihori vyao baada ya kukabidhiwa na Waziri wa Kilimo, Maliasili  Mifugo na Uvuvi, Mmanga Mjengo Mjawiri, hafla iliofanyika huko Kizimkazi Dimbani.
 WAZIRI wa Kilimo, Maliasili  Mifugo na Uvuvi, Mmanga Mjengo Mjawiri, akizungumza na wakulima wa zao la mwani wa Mkoa wa Kusini Unguja, baada ya kuwakabidhi msaada wa vihori, ikiwa ni ahadi ya Serikali ya kuwasaidia wakulima hao ili wawaeze kulima mwani wenye tija katika maji ya bahari  kina kirefu.
 MWENYEKITI wa Masheha Wilaya ya Kusini Unguja,  Ali Haji Mkadam,  akitoa neno la shukurani kwa Serikali, baada ya kukabidhiwa vihori vya kubebea mwani kwa wakulima wa zao hilo ili waweze kulima kilimo chenye tija.
 WAZIRI wa Kilimo, Maliasili  Mifugo na Uvuvi, Mmanga Mjengo Mjawiri, (mwenye kapelo nyeupe) akikibidhi vihori, kwa wakulima wa zao la mwani wa Mkoa wa Kusini Unguja,  ikiwa ni ahadi ya Serikali kuwasaidia wakulima hao  ili waeze kulima mwani wenye tija katika maji ya bahari  kina kirefu, hafla iliofanyika katika uwanja wa mpira Marumbi
 MKURUGENZI Idara ya maendeleo ya Uvuvi, Mussa Aboud Jumbe, (katikati) akizungumza jambo na Waziri wa Kilimo, Maliasili  Mifugo na Uvuvi, Mmanga Mjengo Mjawiri, wakati wa zoezi la ugawaji wa vihori kwa wakulima wa zao la mwani wa Unguja.
WAKULIMA wa zao la mwani wa kijiji cha Marumbi wakiwa wameshikilia vihori vyao baada ya kukabidhiwa na Waziri wa Kilimo, Maliasili  Mifugo na Uvuvi, Mmanga Mjengo Mjawiri hafla iliofanyika uwanja wa mpira Marumbi (PICHA ZOTE NA ABDALLA OMAR). 

No comments:

Post a Comment

ZanziNews Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.