Habari za Punde

Kaskazini Unguja watakiwa kuzingatia suala la amani na utulivu kuelekea uchaguzi mkuu 2020

 Mkuu wa Mkoa wa Kaskazini Unguja Mhe Vuai Mwinyi Mohammed alipofika kukagua vituo vya uandikishaji kuangalia mwenendo wa kazi ya Uandikishaji na uhakiki wa taarifa za Wapiga Kura katika Mkoa huo
 Kwenye vituo vya uandikishaji vimekwa Sanitizer kwa ajili ya usalama wa watakaokuja kujiandikisha

Na Jaala Makame Haji- ZEC

Wananchi wa Mkoa wa Kaskazini Unguja wametakiwa kuzingatia zaidi suala la Amani na Utulivu hasa katika kipindi cha kuelekea katika uchaguzi Mkuu wa mwaka 2020

Mkuu wa Mkoa Kaskazini Unguja Mhe. VUAI MWINYI MOHAMMED alitoa ushauri huo mara baada ya kufanya ziara katika vituo vya uandikishaji yenye lengo la kuangalia mwenendo wa kazi ya Uandikishaji na uhakiki wa taarifa za Wapiga Kura katika Mkoa huo.

Mhe. Mwinyi alisema, suala la kulinda na kudumisha Amani ni la mwananchi, hivyo kuna kila sababu kwa  wananchi kuitunza ili isitoweke na kupelekea athari kwa jamii na taifa kwa ujumla.

Akizungumza kuhusu kazi ya uandikishaji na uhakiki wa taarifa za Wapiga Kura inayoendelea kufanywa na Tume ya uchaguzi ya Zanzibar ZEC katika Mikoa ya Unguja alisema mafanikio ya kazi hiyo yanatokana na matayarisho mazuri na juhudi zilizochukuliwa na Watendaji wa Tume na MAsheha wa Shehia kwa kuwa tayari kuwaelimisha na kuwashajiisha wananchi kushiriki
kikamilifu kati zoezi hilo ambalo ni haki ya kila raia aliyetimiza sifa za kuwemo katika daftari la Kudumu la Wapiga Kura.

Aidha, Mhe. Vuai Mwingi aliwapongeza Tume ya uchaguzi ZEC kwa kazi nzuri wanayoendelea kuifanya kwa kuhakikisha uchaguzi unakuwa huru na wazi kwa kila Mdau wa uchaguzi.

Aliongeza kusema kuwa, ZEC imekuwa ikiwashirikia wadau wa uchaguzi wakiwemo Vyama vya Siasa, Masheha na Makundi Mengine katika kila hatua ya matayarisho ya Uchaguzi mkuu ikiwemo hatua hii ya Uandikishaji na uhakiki wa taarifa za wapiga kura.

Alisifu hatua za tahadhari za kujikinga na maambukizi ya virusi vya CORONA zilizoandaliwa na ZEC katika kila kituo cha uandikishaji.

Nao wakuu wa vituo vya uandikishaji akiwemo Suleiman Mpechi walisema kazi hiyo ya uandikishaji inaendelea vizuri kwani wananchi wanajitokeza kwa wingi katika vituo ili kuomba kuandikishwa ama kuhakikiwa taarifa zao. Kazi ya uandikishaji na uhakiki wa taarifa za wapiga kura
waliokuwemo katika Daftari la Kudumu la Wapiga Kura kwa Mkoa wa Kaskazini Unguja ilimalizika tarehe

No comments:

Post a Comment

ZanziNews Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.