Habari za Punde

Zoezi la ugawaji vyandarua kwa baadhi ya shehia zilizoathirika ma ugonjwa wa Malaria

 Baadhi ya viongozi wa shehia za Wilaya ya Mjini, Magharibi A na Magharibi B walioshiriki zoezi la ugawaji wa vyandarua vilivyotiwa  dawa kwa ajili ya kujikinga na Malaria wakifuatilia uzinduzi huo katika Shehia ya Sogea, Wilya ya Mjini.

 Mkurugenzi Kinga na Elimu ya Afya Dk. Fadhil Mohd akielezea mikakati ya Wizara ya Afya katika kumaliza Malaria Zanzibar wakati wa uzinduzi wa ugawaji wa vyandarua vilivyotiwa dawa katika Shehia ya Sogea, Wilya ya Mjini.
 Naibu Waziri wa Afya Harusi Said Suleiman akiwasisitiza wananchi kutumia vyandarua vilivyotiwa dawa kujikinga na mbu na kuacha tabia ya kuvitumia vyandarua hivyo kwa matumizi mengine wakati wa uzinduzi wa zoezi la kugawa vyandarua uliofanyika Shehia ya Sogea, Wilaya ya Mjini
 Naibu Waziri wa Afya Harusi Said Suleiman akimkabidhi Mkuu wa Wilya ya Mjini Marina Joel Thomas vyandarua ili kuwapa wananchi kujikinga na mbu katika zoezi la ugawaji vyandarua uliofanyika Shehia ya Sogea, Wilaya ya Mjini

Mkuu wa Wilaya ya Mjini Marina Joel Thomas akimkabidhi Sheha wa Shehia ya Sogea Abdalla Mohd Abdalla vyandarua ili kuvigawa kwa wananchi wake katika uzinduzi wa zoezi la ugawaji vyandarua liliofanyika katika Sheia ya ke ya Songea, Wilaya Mjini 

Picha na Ramadhani Ali = Maelezo

Mwashungi Tahir       Maelezo  6/6/2020.
Naibu  Waziri wa Afya Harusi  Said Suleiman ameitaka jamii kuthamini juhudi zinazochukuliwa na Serikali katika kujikinga na malaria kwa kutumia vyandarua vilivyotiwa dawa.
Hayo ameyasema huko katika  Shehia ya Sogea Wilaya ya Mjini  wakati alipokuwa akizindua ugawaji wa vyandarua vilivyotiwa dawa vikiwa na lengo la kujikinga  na malaria kwa  wananchi katika baadhi ya shehia zenye maambukizi.
Amesema Wizara ya Afya  ikishirikiana na Serikali za Wilaya itaendesha zoezi la ugawaji wa vyandarua vilivyotiwa dawa katika baadhi ya shehia ambazo zinaonekana bado zinamambukizi ndani ya Wilaya ya Mjini, Magharib A na Magharib B.   
Hivyo amewaomba wananchi kuvitumia vyandarua hivyo kwa lengo la kujikinga Malaria na kuacha tabia ya kuvitumia kwa mambo mengine ikiwemo kuzungushiwa bustani za mboga mboga.
“Tunawajibu wa kuthamini juhudi za Serikali zinazofanywa kwa wananchi wake ili wawe na afya bora na kutokomeza kabisa maradhi ya malaria kwani iwapo tutakuwa na mashirikiano na kufuata miongozo inayotolewa na Wizara ya Afya Zanzibar bila ya Malaria inawezekana,” alisema Naibu wa Afya.
Amesema wananchi katika shehia nyengine  wataendelea kupata vyandarua  kwa utaratibu wa kuchukua kuponi kwa masheha wao na kwenda katika vituo vyao  vya afya kupatiwa vyandarua.
Pia amesema wagawaji wa vyandarua watazingatia taratibu zote za kujikinga na ugonjwa wa  corona wakati wa zoezi hilo kwa kuvaa barakoa , kutumia vitakasa mikono pamoja na kuvaa glove wakati wote.
Nae Mkuu wa Wilaya ya Mjini Marina Joel Thomas amewaomba masheha kuhakikisha vyandarua hivyo vinawafikia walengwa kwa mpango uliyowekwa na kuwataka wananchi kuvitumia vyandarua hivyo kama vilivyokusudiwa na Serikali.
Kwa upande wake Mkurugenzi Kinga na elimu ya Afya Dk. Fadhil Mohammed amewataka wananchi kufuata miongozo ya Wizara ya Afya kwa kuweka mazingira safi  ili kuepuka  mbu wasizaliane.
Nae Sheha wa shehia ya Sogea Abdullah Mohamed Abdullah na Diwani Mohamed Said Mohamed wamesema watahakikisha wananchi wanavitumia vyandarua hivyo  kujikinga na ugonjwa wa malaria.
Jumla ya vyandarua 197,000 vitagawiwa kwa  kaya 90,000 za wilaya zote tatu  katika shehia 52 zikiwemo shehia 32 Wilaya ya Mjini, shehia 10 Wilaya ya Magharib A na Shehia 10 Wilaya ya Magharibi “B”.
 KUTOKA HABARI MAELEZO

No comments:

Post a Comment

ZanziNews Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.