Habari za Punde

Makamu Mwenyekiti wa Chama Cha ADA-TADEA Mhe. Juma Ali Khatib Achukua Fomu ya kugombea Urais wa Zanzibar

Mgombea Urais wa Zanzibar kupitia Cha cha Ada -TADEA Makamu Mwenyekiti Mhe. Juma Ali Khatib achukua fomu kuomba ridhaa ya Chama chake kupoata nafasi ya kugombea nafasi ya Urais wa Zanzibar  katika uchaguzi Mkuu wa Zanzibar unaotarajiwa kufanyika mwaka huu hafla hiyo imefanyika katika Afisi cha ADA -TADEA Kwa Mchina Jijini Zanzibar, akionesha Mkoba ukiwa na fomu hizo baada ya kukabidhiwa na Naibu Katibu Mkuu wa Chama cha ADA-TADEA Mhe. Rashid Yussuf Mchenga, hayupo pichani  
Naibu kATIBU Mkuu wa Chama cha ADA-TADEA (kulia) Rashid Yussuf Mchenga akimkabidhi Fomu ya kugombea Urais wa Zanzibar Makamu Mwenyekiti wa ADA -TADEA Mhe. Juma Ali Khatib, (kushoto) hafla hiyo imefanyika katika Afisi Kuu ya Chama hicho zilioko Kwa Mchina Jijini Zanzibar. 
Mgombea Urais wa Zanzibar kupitia Chama cha ADA - TADEA Makamu Mwenyekiti wa Chama hicho Mhe. Juma Ali Khatib akitoka katika Afisi za Tadea baada ya kuchukua Fomu ya kugombea Urais wa Zanzibar kupitia Chama hicho. akionesha Mkoba ukiwa na Fomu za kuwania kuteuliwa na Chama chake kukiwakilisha katika Uchaguzi Mkuu wa Zanzibar 
Mgombea Urais wa Zanzibar Makamu Mwenyekiti wa ADA-TADEA Mhe. Juma Ali Khatib akizungumza na waandishi wa habari wa vyombo mbalimbali vilioko Zanzibar baada ya kumaliza zoezi la uchukuaji wa Fomu ya Urais leo katika Afisi za ADA - TADEA Kwa Mchina Jijini Zanzibar.

Mgombea Urais kupitia Chama cha ADA-TADEA Mhe. Juma Ali Khatib akiwaonesha Waandishi wa Habari wa vyombo mbalimbali mkoba wa fomu zake za kugombea Urais wa Zanzibar baada ya kuzungumza nao na kutowa  Sera za Chama Chake kateka kutekeleza iwapo kitapata fursa ya kuchaguliwa.

Baadhi ya Waandishi wa habari wa magazeti wanaofanyika kazi zao Zanzibar  wakifuatilia  sera za mgombea Urais wa Chama cha ADA -TADEA baada ya kuchua fomu leo katika Afisi za Chama hicho Kwa Mchina Jijini Zanzibar.

No comments:

Post a Comment

ZanziNews Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.