Wateja wa Kampuni ya Mawasiliano ya Zantel wakipata huduma katika Duka jipya la Zantel la Vuga baada ya kuboresha na kufanyiwa matengenezo makubwa ili kutowa huduma bora kwa wateja wao. na kuzingatia ushauri wa Wataalam wa Afya.
Mfanyakazi wa Duka la Zantel Vuga Jijini Zanzibar akitowa huduma kwa mtaji wa kampuni hiyo alipofika kupata huduma hiyo.
Zanzibar. Julai 1, 2020. Wateja wa Zantel waliopo Zanzibar
sasa watafurahia kupata huduma za mawasiliano zilizoboreshwa zaidi katika duka jipya la
Zantel lililopoVuga Jijini baada ya kufanyika kwa maboresho ili kukidhi mahitaji ya wateja.
Duka hilo
la kisasa limezingatia pia
afya za wateja kwa kuwekewa miundombinu mbalimbali kwa ajili ya kuendelea kuchukua tahadhari dhidi ya maambukizi ya ugonjwa wa
Corona (Covid-19) ikiwamo sehemu maalumu za kuoshea mikono pamoja na ukaaji foleni wa kuzingatia umbali wa mita mbili.
Akizungumza wakati wa uzinduzi huo,
Mkuu wa Zantel - Zanzibar.Ndg. Mohamed Khamis Mussa Baucha alisema duka hilo lenye zaidi ya miaka
20 limeboreshwa kuendana na mabadiliko ya kiteknolojia ili kukidhi mahitaji ya huduma kwa wateja
wake.
“Hili duka tumelifanyia ukarabati wa hali ya juu ili liwe imara na tumeliimarisha katika nyanja zote. Sisi mara zote tunasikiliza kero za wateja wetu na moja ya kero ilikuwa ni foleni hivyo tumeleta mfumo maalumu wa kukaa kwenye foleni
(Queuing system) ambao utapunguza msongamano,” alisema.
Mfumo huo unaruhusu mteja kujisajili kwenye mtambo maalum na kupewa namba atakayoitumia wakati anasubiri huduma kwenye foleni na ataitwa mara tu zamu yake itakapofika hali inayofanya kuwa na ufanisi wa huduma.
Vile vile,
duka hilo linauwezo wa kutoa huduma kwa wateja zaidi ya 100
kwa siku na kwamba kwa maboresho hayo wataweza kuhudumia wateja wengi zaidi kwa haraka zaidi.
“Nategemea tutahudumia wateja wengi zaidi kwa haraka kwa hiyo nawakaribisha wateja waje wajionee duka jipya na
la kisasa ambalo ni duka la kwanza la Zantel Unguja,” alisema Meneja wa Maduka ya Zantel Zanzibar.Bi. Mwajuma Senkanga.
Huduma zinazopatikana dukani hapo ni pamoja na huduma ya Ezypesa,
kusajili namba za simu, pamoja na bidhaa za mawasiliano kama vile simu.
Zantel
ni Kampuni inyaoongoza kwa utoaji wa huduma za mawasiliano Visiwani Zanzibar
kwa miaka mingi hivi sasa ikiongoza kwa ubora wa miundombinu ya mawasiliano,
huduma pamoja na bidhaa.
Huduma ya kifedha ya Ezypesa ni ya
kwanza nchini Tanzania
kutoa huduma za kibenki za kawaida pamoja na za kiislamu kwa ushirikiano na benki ya Watu wa
Zanzibar (PBZ).
Aidha, Zantel ni kampuni inayoongoza kwa utoaji wa huduma za intaneti nchini
Tanzania kupitia uwekezaji kwenye teknolojia ya fibre optic cable
ambayo inaiunganisha Tanzania
na nchi nyingine za Afrika Mashariki na duniani umeiwezesha Kampuni hiyo kuleta mapinduzi ya haraka ya kidigitali hapa nchini.
Aidha, Miundombinu hiyo imeiwezesha
Zantel kutoa huduma za kimataifa za sauti na data
kwa jumla kwa kampuni nyingine na nchi jirani hivyo kuchagia ukuaji wa teknolojia ya digitali.
No comments:
Post a Comment