Habari za Punde

Zantel Yatiliana Saini na Wakala wa Miundombinu ya Mawasiliano (TEHAMA) Kuboresha Mawasialiano Kisiwani Pemba.

Naibu Waziri Wizara ya Ujenzi Mawasiliano na Usafirishaji Zanzibar Mhe Mohammed Ahmada (katikati)  akishuhudia utiaji wa Saini baina ya Kampuni ya Simu ya Zantel Zanzibar ikiwakilishwa na Mkuu wa Zantel Zanzibar Ndg. Mohammed Mussa Baucha (kushoto kwa Waziri) na (kulia kwa Waziri) Mkurugenzi wa Wakala wa Miundombinu ya Mawasiliano (Tehama), Mhandisi Shukuru Suleiman, kuunganishwa kwenye mkongo wa Taifa kati ya Pemba na Tanga kuboresha mawasiliano kisiwa cha Pemba,
Naibu Waziri  Wizara ya Ujenzi Mawasiliano na Usafirishaji Zanzibar Mhe. Mohammed Ahmada akishuhudia makabidhiano ya mkataba wa kuunganishwa kwenye mkongo wa Taifa kati ya Pemba na Tanga kuboresha mawasiliano kisiwa cha Pemba, wakitia Saini Mkuu wa Zantel-Zanzibar,Ndg. Mohammed Mussa Baucha na (Kulia) Mkurugenzi wa Wakala wa Miundombinu ya Mawasiliano (Tehama), Mhandisi Shukuru Suleiman (kushoto).Hatua hiyo itasaidia kuboresha huduma za mawasiliano visiwani humo.


No comments:

Post a Comment

ZanziNews Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.