Habari za Punde

Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Mhe.Dk. Ali Mohamed Shein Ameweka Jiwe la Msingi Jengo la Ofisi la ZSSF Tibirinzi Pemba.

Muonekano wa Jengo la Ofisi za Mfuko wa Hifadhi ya Jamii Zanzibar ZSSF linaloendelea na Ujenzi wake katika hatua za mwisho lilioko katika eneo la Tibirinzi Chakechake Pemba.

RAIS wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Mhe.Dk. Ali Mohamed Shein, akisalimiana na Mkurugenzi Mkuu wa Mfuko wa Hifadhi ya Jamii Zanzibar (ZSSF) Bi. Sabra Issa, alipowasili katika viwanja vya Tibirinzi kuhudhuria hafla ya uwekaji wa Jiwe la Msingi  Jengo la Ofisi za ZSSF linalojengwa katika eneo la Tibirinzi Wilaya ya Chakechake Pemba.

Waandishi wa habari wa vyombo mbalimbali Pemba wakifuatilia hafla ya Uwekaji wa Jiwe la Msingi Jengo kla Ofisi za ZSSF Tibirinzi Wilaya ya Chakechake Pemba. 
RAIS wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Mhe.Dk. Ali Mohamed Shein, akiondoa kipazia akiweka Jiwe la Msingi la Jengo la Ofisi za Mfuko wa Hifadhi ya Jamii Zanzibar (ZSSF) linalojengwa katika eneo la Tibirinzi Chakechake Pemba hafla hiyo imefanyika leo 5/8/2020 na (kulia kwa Rais) Mkurugenzi Mkuu ZSSF Bi. Sabra Issa.

RAIS wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Mhe.Dk. Ali Mohamed Shein, akifurahia jambo na Waziri wa Fedha na Mipango Zanzibar Mhe. Balozi Mohammed Ramia Abdiwawa na (kulia kwa Rais) Mkurugenzi Mkuu wa Mfuko wa Hifadhi ya Jamii Zanzibar (ZSSF) Bi. Sabra Issa, baada ya uwekaji wa Jiwe la Msingi  Jengo la Ofisi za ZSSF linalojengwa katika eneo la Tibirinzi Wilaya ya Chakechake Pemba.
RAIS wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Mhe.Dk. Ali Mohamed Shein, akimsikiliza Meneja Mipango, Uwekezaji na Utafiti ZSSF Ndg. Abdulazizi Ibrahim Iddi, wakati wa hafla ya Uwekaji wa Jiwe la Msingi la jengo la Ofisi la ZSSF linalojengwa katika eneo la Tibirinzi Chakechake Pemba

RAIS wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Mhe.Dk. Ali Mohamed Shein, akipata maelezo kutoka kwa Mkurugenzi Mkuu wa Mfuko wa Hifadhi ya Jamii Zanzibar (ZSSF) Bi. Sabra Issa, alipokuwa akitembelea jengo hilo baada ya kuweka jiwe la msingi na (kulia kwa Rais) Spika wa Baraza la Wawakilishi Zanzibar Mhe. Zuberi Ali Maulid , lilioko katika eneo la Tibirinzi Wilaya Chakechake Pemba.
RAIS wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Mhe.Dk. Ali Mohamed Shein akizungumza na Wananchi wa Tibirinzi wakati wa hafla ya Uwekaji wa Jiwe la Msingi Jengo la ZSSF Chakechake Pemba 
WANANCHI wa Tibirinzi Chakechake Pemba wakimsikiliza Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Mhe. Dk. Ali Mohamed Shein,(hayupo pichani) akiwahutubia baada ya uwekaji wa jiwe la Msingi la Jengo la ZSSF 
RAIS wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Mhe.Dk. Ali Mohamed Shein akiwa katika picha ya pamoja na Viongozi wa Serikali na Wafanyakazi wa ZSSF baada ya kumalizika kwa hafla ya uwekaji wa jiwe la msingi Jengo la ZSSF Tibirinzi Wilaya ya Chakechake Pemba.

No comments:

Post a Comment

ZanziNews Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.