Habari za Punde

Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk. Shein Aweka Jiwe la Msingi Jengo la Ofisi za ZRB Gombani Pemba.

 RAIS wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Mhe.Dk. Ali Mohamed Shein, akiondoa kipazia kuashiria kuweka Jiwe la Msingi la ujenzi wa Jengo linalojengwa katika eneo la Gombani Chakechake Permba na (kushoto kwa Rais) Kamishna wa Bodi ya Mapato Zanzibar (ZRB) Ndg. Joseph Abdalla
 MUONEKANO wa Jengo  la ZRB Gombani Pemba lililowekwa jiwe la Msingi na Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Mhe.Dk. Ali Mohamed Shein(yayupo pichani) hafla hiyo imefanyika
 RAIS wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Mhe.Dk. Ali Mohamed Shein, akimsikiliza Mshauri Mkuu Elekezi wa Ujenzi wa Jengo la ZRB Gombani Chakechake Pemba Ndg. Oswald Modu, wakati wa hafla ya uwekaji jiwe la msingi la jengo uliofanyika leo 5/8/2020.

RAIS wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Mhe.Dk. Ali Mohamed Shein, akitembelea ujenzi wa Jengo la ZRB Gombani Pemba wakati wa hafla ya uwekaji wa Jiwe la Msingi la Jengo hilo,(kushoto kwa Rais) Mwenyekiti wa Bodi ya ZRB Ndg. Saleh Sadiq na (kulia kwa Rais) Kamishna wa Bodi ya Mapato Zanzibar  ZRB. Ndg Joseph Abdalla Meza, wakati akitembelea ujenzi huo baada ya kuweka jiwe la msingi 

No comments:

Post a Comment

ZanziNews Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.