Habari za Punde

Mgombea Urais wa Zanzibar Kwa Tiketi ya CCM Mhe.Dk. Hussein Mwinyi Anguruma Pemba Katika Mkutano Wake wa Kampeni Gando.Wilaya ya Wete.

Mgombea Urais wa Zanzibar kwa tiketi ya Chama Cha Mapinduzi Mhe.Dk. Hussein Mwinyi akiwahutubia Wananchi wa Wilaya ya Wete Pemba katika mkutano wake wa Kampeni uliofanyika katika Uwanja wa mpira Gando na kuwaomba Kura Wananchi wa Pemba na kuwaombea kura Wagombea Ubunge, Uwakilishi na Udiwani wa CCM.

Na. Mwandishi Wetu Pemba. 

MGOMBEA wa nafasi ya urais wa Zanzibar kupitia Chama Cha Mapinduzi(CCM) Dk.Hussein Ali Mwinyi amesema akipata ridhaa ya kuiongoza Zanzibar serikali yake atakayoiongoza itahakikisha inatoa pembejeo kwa wakulima ili kuongeza uzalishaji wa mazao kwa wakulima na wenye tija visiwani hapa.

 

Amesema ataweka kipaumbele cha aina yake kwenye eneo hilo la utoaji wa pembejeo katika kilimo cha karafuu,mpunga na viuongo ili wakulima wanufaike kwa namna moja ama nyingine.

 

Kauli hiyo ameitoa jana wakati akihutubia katika kampeni alizozifanya kwenye kijiji cha Gando wilaya ya Wete mkoa wa Kaskzaini Pemba ambapo alisema lengo la kuweka kipaumbele hicho cha utoaji wa pembejeo ni kuhakikisha wakulima wanazalisha kwa tija ikilinganishwa na kilimo kinacholimwa kwa sasa.

 

Alisema serikali ya awamu ya saba ya CCM imefanya mambo mengi ikiwemo kuwawezesha wakulima wa mwani kwa kuwapatia vihori 80 wakulima wa mwani wa wilaya ya Wete na kwamba yote wananchi wa wilaya hiyo wanatambua hilo.

 

"Miundombinu ya kilimo cha umwagiliaji yenye urefu wa kilomita 193 katika maeneo mbalimbali ya wilaya hii ya Wete na hii imetoa fursa kwa wakulima kupata tija zaidi katika shughuli zao,"alisema

 

Alisema katika eneo la kilimo imetolewa ruzuku kwa wakulima zaidi ya asilimia 75 ya pembejeo mbalimbali katika kilimo cha mpunga.

 

"Ndugu zangu haya yote yamefanywa na serikali ya CCM na hatuna wasiwasi wowote kuwa ilani ya uchaguzi ya CCM imefanyika vizuri katika kipindi cha miaka 10 ya serikali ya awamu ya saba,"alisema     

 

Dk.Mwinyi alisema kwa upande wa kilimo cha karafuu ambacho ndio zao kuu Zanzibar zao la biashara visiwani hapa ambapo kiwango cha uzalishaji kimeongezeka kutoka tani 3321 kwa mwaka 2015 hadi tani 8277 kwa mwaka 2018.

 

"Hizi zote ni juhudi za serikali ya CCM ya kutoa miche na pembejeo kwa wakulima na kuongeza uzalishaji katika zao kuu la biashara kuu Zanzibar,"alisema 

 

Akimnadi mgombea huyo Makamu Mwenyeki wa CCM ambaye pia ni Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi DK. Ali Mohaemmed Shein amesema, visiwa vya Zanzibar vinahitaji rais ambaye atayaenzi na kuyalinda mapinduzi matukufu ya mwaka 1964.

 

Amesema, lazima Mapinduzi yaenziwe na yatunzwe na Chama cha Mapinduzi pekee ndicho ambacho kinaleta rais na viongozi ambao watayaenzi mapinduzi hayo.

 

Rais Dk. Shein alisema CCM inapoamua kuleta wagombea wake huleta wagombea mahiri, wenye uwezo wa kuijenga Zanzibar na kuiendeleza.

"Watu wengine wanaleta mzaha na wanataka kujaribu urais ila niwaambie tu urais haujaribiwi, hapana kujaribu dola, uamuzi ni mmoja tu chagueni chama cha Mapinduzi," alisema.

 

DK.Shein alisema, urais ni heshima kubwa katika taifa lolote hivyo sio jambo la kujaribu kwa sababu tu kila mtu ana hamu ya kuwa rais.

 

Alisema, Chama cha Mapinduzi kimemchagua DK. Hussein Ali Mwinyi kuwa mgombea urasi kwa sababu ya ukweli wake, uaminifu wake na uungwana wake.

 

"DK. Mwinyi anauwezo mkubwa sana, tusibabaishwe maana kila mtu anasema yake ila nataka niwaambie ukweli DK. Mwinyi yupo tofauti na wagombea wengine," alisema.

 

Alisema, Chama cha Mapinduzi hakiwezi kuchagua viongozi ambao hawana uwezo, ambapo kuanzia wabunge, wawakilishi, madiwani na rais wote wanachaguliwa wenye uwezo mkubwa.

 

"Msibabaike ndugu zangu wa Gando mwaka huu fanyeni uamuzi wa busara, nyinyi kama hamfanyi watafanya wa majimbo mengine alafu nyinyi mtakuja kununa hivyo niwaombe mfanye uamuzi wa busara wa kukichagua Chama cha Mapinduzi," alisema.

 

Mbali na hayo, DK. Shein aliendelea kumnadi na kuelezea sifa za Magombea urasi wa Zanzibar kupitia CCM, DK. Hussein Ali Mwinyi na kusema, DK. Mwinyi anasifa za kuwa kiongozi bora na uwezo mkubwa.

 

Alisema, DK. Mwinyi ni kiongozi mahiri sana mwenye sifa zote za kuwa rais wa Zanzibar.

"Na mimi nnapokuwa nayasema haya nasema kwa dhati ya moyo wangu, kwa sababu mimi ndiyo rais wa Zanzibar sasa hivi kwahiyo naujua urais, nazijua kazi za urasi zilivyo,

 

hivyo bila shaka majukumu haya dk Mwinyi anaweza kutafaya kwa asilimia 100," alisema.

 

Kwa upande wake Naibu Katibu mkuu wa Chama cha Mapinduzi Zanzibar DK. Abdullah Juma Sadala (Mabodi) alisema, chama cha Mapinduzi kinaendelea kunadi sera zake na kuelezeayale yote ambayo yamefanikiwa katika awamu iliyopita.

 

Akizungumzia utekelezaji wa ilani ya Chama cha Mapinduzi, katika wilaya ya Wete alisema kuna mambo mengi ambayo yametekelezwa katika uongozi wa DK. Shein ikiwa ni pamoja na kupata umeme vijijini, lakini pia kujengwa kwa barabara kwa kiwango cha lami.

 

Lakini pia alisema, serikali ya CCM imefanikiwa pia katika swala zima la elimu na kwa upande wa afya katika wilaya hiyo serikali imejenga vituo vipatavyo 10, lakini pia imenunua boti ya kubebea wagonjwa baharini, ambapo wagonjwa kutoka katika visiwa vidogo vidogo wanapata nafasi ya kupelekwa katika hospitali ya rufaa kwa haraka.

Mwenyekiti wa Chama cha Mapinduzi mkoa wa Kaskazini Pemba kichama, Mberwa Juma Mberwa alimpongeza Dk. Shein kwa kipindi chake chote cha uongozi wenye mafanikio tele kwa kipindi cha miaka 10.

 

Lakini alimuomba Rais huyo kuendelea kutoa mashirikiano na ushauri wakati ambao atakuwa tayari amestaafu ili chama cha Mpainduzi kiendelee kuwa imara.

 

Mbali na hayo aliwataka wananchi wa mkoa wa Kaskazini Pemba kuwapa kura wagombea wote wa Chama cha Mapinduzi kuanzia Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Rais wa Zanzibar pamoja na wabunge, wawakilishi na madiwani wote wa Chama cha Mapindzi.

 

 

Katika mkutano huo wa kampeni uliofanyika katika kijiji cha Gando, Rahama Hamad jana alirejesha kadi ya chama cha ACT-Wazalendo na kujiunga na CCM ambapo alisema yeye anaishi wilaya ya Wete mkoa wa Kaskazini Pemba na kwamba kwa dhamira yake mwenyewe ameamua kurudisha kadi hiyo na kurudi nyumbani alipokuwa awali.

 

Alisema amekuwa na dukuduku kwa kipindi cha muda mrefu na kwamba hatua hiyo ndio imemsababishia arudi kujiunga na CCM ambapo amewaomba wanachama waliojitokeza katika mkutano huo kuwa atatumia nafasi kwenye mikutano mingine ya kampeni kwa siku zingine kwa ajili ya kuwalipua viongozi wa upinzani wa chama alichotokea.

 

Rahama alisema kutokana na muda uliopo kwenye mkutano huo hautoshi amewataka wanachama hao kuwa na subra na kuamua kutumia mikutano mingine ya kampeni ambayo CCM inaendelea kufanya ya kuwanadi wagombea wa nafasi za Ubunge,Uwakilishi na Udiwani katika maeneo mbalimbali ya wilaya ya Wete mkoa wa Kaskazini Pemba.

 

           

 

Kwa upande wake Naibu Katibu Mkuu wa CCM Zanzibar Dk. Abdullah Juma Sadala 'Mabodi' alisema CCM  kinaendelea kunadi sera zake na kuyaeleza mambo yote ambayo yamefanikiwa kuyatekeleza katika kipindi cha miaka 10 chini ya serikali ya anayoiongoza Rais Dk.Shein.

 

Akizungumzia utekelezaji wa ilani ya CCM  katika wilaya ya Wete mkoa wa Kaskazini Pemba ambapo alisema kuna mambo mengi ambayo yametekelezwa katika uongozi wa Rais Dk. Shein ikiwemo kupatikana kwa uwakika wa huduma za nishati za umeme kwenye vijiji pamoja na kujengwa kwa barabara kwa kiwango cha lami.

 

Naibu Katibu Mkuu huyo alisema, serikali ya CCM imefanikiwa kutekeleza kwa kijiji hicho cha Gando katika suala la elimu huku kwa upande wa afya katika wilaya ya Wete serikali imejenga vituo 10 ya afya na kwamba pia imenunua boti ya dharura ya kubebea wagonjwa baharini ambapo wagonjwa kutoka katika visiwa vidogo vidogo wanapata urahisi wa  kupelekwa katika hospitali ya rufaa kwa haraka.

 

Kwa upande wake Mwenyekiti wa CCM mkoa wa Kaskazini Pemba, Mbelwa Hamad Mbelwa alimuhakikishia Makamu Mwenyekiti wa CCM Taifa, Rais Dk.Shein kuwa uongozi wa mikoa miwili ya CCM ya Kusini na Kaskazini Pemba inashirikiana vyema katika kuhakikisha kuwa chama kinapata ushindi wa kishindo kwenye uchaguzi mkuu unaotarajiwa Oktoba 28 mwaka huu.

Alisema CCM mkoa wa Kaskazini Pemba ipo salama na kwamba inaendelea vyema na wana imani kuwa ya kuwa chama kitapata ushindi hivyo mkoa huo unawaombea kura wagombea wote wa CCM katika nafasi ya urais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Rais Dk.John Magufuli pamoja na mgombea wa urais wa Zanzibar Dk.Hussein Ali Mwinyi na wagombea wa nafasi ya Ubunge,Uwakilishi na udiwani.

 

"Makamu Mwenyekiti Taifa ninaomba kwanza nitoe pongezi kwa niaba ya mkoa wa Kaskazini kwa kipindi chote cha miaka 10 ya uongozi wako hivyo baada ya pongezi hizo jambo lingine tunakuomba wakati ukishamaliza kipindi chako cha uongozi tunaomba usisite kutufungulia mlango tukija kuchota busara zako na ushauri zako ili kukiendeleza CCM,"alisema

No comments:

Post a Comment

ZanziNews Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.