Habari za Punde

Mkurugenzi Mtendaji wa Benki ya CRDB Ndg Nsekela Akiwasilisha Mada Katika Semina na Viongozi Waandamizi na Wajumbe wa Baraza la Wawakilishi Zanzibar.

MKURUGENZI Mtendaji wa Benki ya CRDB Tanzania Ndg. Abdulmajid Mussa Nsekela akiwasilisha Mada ya Maendeleo ya Benki ya CRDB kwa Washiriki wa hafla hiyo Viongozi Waandamizi na Wajumbe wa Baraza la Wawakilishi Zanzibar, iliofanyika katika viwanja vya Marina Hoteli ya Verde Mtoni Jijini Zanzibar jana usiku 28/11/2020

Mkurugenzi Mtendaji wa Benki ya CRDB Abdulmajid Nsekela akiwasilisha mada juu ya shughuli za Benki hiyo na jinsi ilivyojipanga katika kushirikiana na Serikali ya Awamu ya Nane na kueleza kwamba Benki hiyo iko tayari na kumuomba Rais aipe timu kwa ajili ya kufanya kaziili kuleta maendeleo ya kasi na chanya.

Alisema kwamba Benki ya CRDB imedhamiria kufanyakazi kwa karibu zaidi na Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar Awamu ya Nane ikidhamiria kuunga mkono katika kujenga uchumi imara wenye kutegemea rasilimali za bahari yaani “Uchumi wa buluu”.

"Tunafahamu Serikali ya Awamu ya Nane imejipanga kuleta Mapinduzi katika sekta zote za maendeleo na sisi tumeweka mkakati wa ushiriki wetu kuanzia sekta ya utalii, kilimo, uvuvi, ujenzi, viwanda, miundombinu, elimu na afya” alisema Nsekela huku akibainisha kuwa uwezeshaji huo unafanyika kuanzia kwa wajasiriamali wadogo, wakati na kwa makampuni makubwa.

Alisisitiza kwamba Benki ya CRDB imejidhatiti vya kutosha katika kutoa mikopo ya maendeleo usahili wa Mfuko wa Umoja wa Mataifa wa Tabia nchi (GCF) ulioipata Benki hiyo mwishoni mwa mwaka jana umesaidia kwa kiasi kikubwa kuongeza uwezo wa benki hiyo kutoa mikopo ambapo sasa hivi inaweza kutoa hadi dola za kimarekani milioni 250 kwa mradi mmoja.

“Hizi ni fedha nyingi sana ambazo tumedhamiria kuzielekeza katika miradi ya maendeleo nchini kwa kushirikiana na Serikali na sekta binafsi,” aliongezea Nsekela.

Aidha Nsekela alisema Benki ya CRDB inaendelea na zoezi la uunganishwaji wa mfumo wa kidijitali wa malipo katika taasisi za Serikali na binafsi ili kuongeza ufanisi katika ukusanyaji wa mapato.“tunafanya hivi tukiwa na uzoefu wa kuisaidia Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar kukusanya mapato katika sekta ya utalii ambapo zilikukusanywa fedha zinazofikia dola za kimarekani milioni 12 mwaka 2019 kutoka dola laki 4 mwaka 2014,” alisema Nsekela.

Mkurugenzi huyo alieleza azma ya Benki yake kutoa ushirikiano kwa Serikali ya Awamu ya Nane ili kuifanya Zanzibar kuwa Dubai yakesho sambambana kuonesha utayari wake kwa kusaidiana naS erikali kutafuta wawekezaji kuja kuekeza Zanzibar.

Benki ya CRDB inamatawi mawili Zanzibar ambapo moja lipo Unguja na jingine Pemba ambapo benki hiyo pia, imefanikiwa kupanua wigo wake wa huduma kupitia CRDB, Wakala zaidi ya 160 ambao wanasadia kutoa huduma kwa Wazanzibari zaidi ya 300,000 na tayari mikopo ya benki hiyo hapa Zanzibar imefikia shilingi bilioni 101 ambazo zimekopeshwa katika maeneo mbali mbali huku wadau wake kwa asilimia 80 ni Watanzania.

No comments:

Post a Comment

ZanziNews Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.